Fadhila za (laailaha ila Allah)

Fadhila za (laailaha ila Allah)

Fadhila za (laailaha ILA Allah)

Amesema Mtume Wa Allah (S.A.W) “ Umejengwa Uislamu Kwa Mambo Matano: Kushudia Kuwa Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Isipokuwa Allah, Na Muhamad Ni Mtume Wake , Na Kusimamisha Swala Na Kutoa Zaka Na Kuhiji Na Kufunga Mwezi Wa Ramadhani” (Amepokea Bukhari)

Akasema Tena Mtume (S.A.W) &" Neno Bora Nililolisema Mimi Na Manabii Wote Walionitangulia Ni: (Laailaha Ila Allah Wahadahu Laasharika Lahu Lahu-L Mulku Walahu-L Hamdu Wahuwa Aalakuli Shain Qadiir)Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah Peke Yake Hana Mshirika, Ufalme Ni Wake Na Sifa Njema Zake Naye Ni Muweza Wa Kila Kitu. &" (Imepokewa Na Atirmidhiyu)

‘Laailaha Ila Allah’, Kwa Ajili Yake Alipamba Allah Pepo Na Kuchochea Moto Kisha Akaweka Soko La Mambo Mema Na Maovu.

Akasema Mtume (S.A.W) &" Hakika Mtume Nuuh (A.S) Alipojiwa Na Umauti Akamwambia Mwanawe: Nina Kuamrisha Kwa ‘Laailaha Ila Allah’ Kwasababu Kama Itachukuliwa Laailaha Ilaha Ila Allah, Nakuwekwa Kwenye Mizani Na Mbingu Saba Na Ardhi Saba Sehemu Nyingine Ya Miizani, Basi Laailaha Ila Allah Itakuwa Nzito Na Kuangusha Sehemu Ya Pili Ya Mizani, Na Kama Ingelikuwa Mbingu Saba Na Ardhi Saba Ni Kama Pete Isiyojulikana Lailaha Ila Allah Itazishinda Nguvu.&" (Imepokewa Na Bukhari Katika Kitabu Chake Aladabu L- Mufrad)

MASHARTI YA ‘LAAILAHA ILA ALLAH’

1-Elimu Kwa Maana Yake : Nayo Ni Kutambua Mwenye Kuitamka Kalma Hii Ayajue Maana Yake Na Madhumuni Yake Na Vilivyo Ambatana Nayo Miongoni Mwavyo Kukanusha Uungu Wa Asiye Kuwa Allah Nakuuthibitisha Kwake Allah, Amesema Allah Mtukufu: { Jua Ya Kwamba Hakuna Aabudiwaye Kwa Haki Ila Mwenyezi Mungu } (Muhamad : 19)

2-Al-Yaqin : Maana Yake Nikwamba Isipatikane Shaka Yoyote Kwa Mwenye Kutamka Kalima Hii Juu Ya Kalima Yenyewe Au Juu Ya Vinavyo Ambatana Navyo.Kwa Kauli Yake Allah Aliyetukuka { Wenye Kuamini Kweli Kweli Ni Wale Waliomuamini Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake;Kisha Wakawa Si Wenye Shaka,Na Wakaipigania Dini Ya Mwenyezi Mungu Kwa Mali Na Nafasi Zao Hao Ndio Wenye Kuamini Kweli. } (Al-Hujurat: 15)

Na Akasema Mtume (S.A.W) ‘ Nashuhudia Kuwa Hakuna Aabudiwae Kwa Haki Ila Allah Na Mimi Ni Mtume Wake Hakuna Atakaye Kutana Na Allah Na Kalima Hii Asiwe Na Shaka Juu Yake Isipokuwa Allah Atamuingiza Peponi.’ (Imepokewa Na Muslim)

3-Kukubali Yaliyo Ambatana Na Hii Kalima Kwa Moyo Na Ulimi: Na Maana Ya Kukubali Hapa Ni Kinyume Cha Kupinga Na Kujivuna Amesema Allah Mtukufu: {Hivyo Ndivyo Tutakavyowafanya Maasi. Wao Walipokuwa Wakiambiwa, Hakuna Aabudiwaye Kwa Haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu,”Walikuwa Wakikataa. } (As-Saaffat: 34-35)

4-Kufuata Yaliyoelekezwa Na Kalima Ya Tawheed : Kwa Maana Mja Awe Anatekeleza Aliyo Amrishwa Na Allah Na Kuachana Na Yote Aliyokatazwa, Amesema Allah Mtukufu : { Na Ajisalimishaye Uso Wake Kwa Mwenyezi Mungu, Na Hali Ya Kuwa Anawafanyia Mema (Viumbe Wenziwe), Bila Shaka Amekwishakamata Fundo Lililo Madhubuti;Na Mwisho Wa Mambo Yote Ni Kwa Mwenyezi Mungu } (Luqman :22)

Hakika Utumwa Wa Kweli Ni Utumwa Wa Moyo, Basi Mwenye Kuumiliki Ndiye Atakuwa Bwana Wa Moyo Huo Nao Utakuwa Mtumwa Kwake.

5-Ukweli: Maana Yake Ni Aitamke Mwenye Kutamka Kalima Kwa Ukweli Kabisa Ndani Ya Moyo Wake, Moyo Wake Ayasemayo Yawafiki Yaliyomo Moyoni Mwake. Amesema Allah Mtukufu: {Na Katika Watu, Wako (Wanafiki) Wasemao: “Tumemuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho”; Na Hali Ya Kuwa Wao Si Wenye Kuamini. Wanatafuta Kumdanganya Mwenyezi Mungu Na Wale Walio Amini, Lakini Hawadanganyi ILA Nafsi Zao; Nao Hawatambui} (Al Baqarah: 8-9)

6-Ikhlaas ( Kumtakasia Allah Ibada) : Nayo Ni Kutaka Radhi Za Allah Katika Kalima Ya Tawhiid, Amesema Allah Mtukufu: { Wala Hawakuamrishwa Ila Kumwabudu Mwenyezi Mungu Kwa Kumtakasia Dini, Waache Dini Za Upotevu, Na Wasimamishe Sala Na Kutoa Zaka- Hiyo Ndiyo Dini Iliyo Sawa. } (A-L Bayyinah: 5)

7-Kuipenda Kalima Hii Ya Tawhiid Na Kuwapenda Watu Wake Wenye Kuifanyia Kazi Na Wenye Kushikamana Nayo, Kwa Sharti Zake, Na Kumbughudhi Kila Mwenye Kuikanusha . Amesema Allah Mtukufu: {Na Katika Watu Wapo Wanao Chukua Waungu Wasio Kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda Kama Kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini Walio Amini Wanampenda Mwenyezi Mungu Zaidi Sana. } {Al-Baqarah: 165}

Hii Ndio Maana Ya (Laailaha ILA Allah) Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki ILA Allah, Na Hizo Ndizo Sharti Zake Ambazo Kwazo Zitakuwa Ni Sababu Ya Kufuzu Mbele Ya Allah. Aliambiwa Hassan Albasriy: Hakika Watu Wanasema : Mtu Akisema Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah, Ataingia Peponi , Akasema Mwenye Kusema Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah Na Akatekeleza Haki Zake Na Faradhi Zake Ataingia Peponi”

Kila Moyo Ukiongezeka Mapenzi Yakumpenda Allah Huzidi Kumuabudu Na Kuwa Mja Wake Halisi Na Kuwa Huru Na Miungu Wengine Wote.

Kwa Hiyo Kalima Hii Ya Tawhiid Haimfaidishi Mwenye Kuisema Isipokuwa Aifanyie Kazi Kwa Kuleta Sharti Zake, Lakini Mwenye Kuitamka Bila Kuifanyia Kazi Basi Haimnufaishi Na Lolote Mpaka Atakapo Leta Vitendo Viambatane Na Maneno Yake.Tags: