ATHARI ZA KAWAIDA KWA WATUWOTE

ATHARI ZA KAWAIDA KWA WATUWOTE

Kama zilivyo dhihiri athari za tawhiid na imani kwenye moyo wa muumini, na katika mwenendo wake na tabia zake, zadhihiri vilevile katika mwenendo wake na tabia zake kwa watu wengine. Amesema Mtume [s.a.w]«Hakika mimi nimetimilizwa kukamilisha tabia njema»(Imepokewa na Albaihaqi)

Bali Mtume [s.a.w] alikusanya baina ya imani na tabia nzuri aliposema: «Muumini aliye kamilika imani yake ni Yule aliye na tabia nzuri na aliye na ulimi laini kwa watu wake [wake zake»(Imepokewa na Atirmidhi)

Mwenye kumpwekesha Allah ambaye anachunga kuonekana na Allahhamu kuenea elimu yake Allah kwa viumbe wake, mtu huyu atakuwa na huruma sana na kusikitikia sana watu wenzake katika Nyanja nyingi maishani mwake.

Nyumbani na familia

 1. kuamiliana na wazazi

Muislamu anayempwekesha Allah, ni mwingi sana wa kuchunga haki za wazazi wawili, Allah alieka baada ya haki yake ni kuwatekelezea haki zao, ndani ya qurani , aliposema: {Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila yeye tu. Na kuwafanyia wema wazazi . Kama mmoja wao akifikia uzee, na yuko pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa [njia ya kuwaonea] huruma na sema. Mola wangu! Warehemu [wazee wangu] kama walivyonilea katika utoto,’. Mola wenu anajua sana yaliyo nyoyoni mwenu. Kama mkiwa wema kwani yeye ni Mwenye kuwaghufiria wenye kurejea [kwake]} [Al-israi :23-25]

Na amesema tena Allah Mtukufu “Na tumemwusia mwanadamu afanye wema kwa wazazi wake; na kama wakikushurutiza kunishirikisha na yale usiyo na ilmu nayo, basi usiwatii; kwangu ndiyo marejeo yenu, basi nitakwambieni mliyokuwa mkiyatenda.} [Al-ankabuut : 8]

 1. Kuamiliana na watoto

Ijapokuwa watoto ni pambo la dunia, anasema Allah kuwahusu: {Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia} [Al-kahfi: 46]

Ispokuwa tawheed ilioko moyoni mwa muislamu inamwita kuwalea watoto wake, na inamwelekeza jinsi ya kuwalea hao watoto. Na Allah aliwalingania waumini kwa imani yao kuzilinda nafsi zao na za jamaa zao kutokana na moto wa jahanam, akasema Allah {Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu, na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake; na wanatenda wanayoamrishwa [yote]} [At-tahrim: 6]

Akajaalia majukumu kwa kila mchunga, akasema Mtume[s.a.w] «Hakika nyinyi nyote ni wachunga na nyote mtaenda kuulizwa mlivyo vichunga, Kiongozi ni mchunga na ataenda kuulizwa aliowachunga, na mtu mzima ni mchunga kwa watu wa nyumbani mwake na ataenda kuulizwa aliowachunga, na mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mumewe na ataenda kuulizwa alivyovichunga, na yaya wa nyumbani ni mchunga wa mali ya bwana wake na ataenda kuulizwa alivyovichunga» (Imepokewa na Albukhari)

 1. kuamiliana na mke

Muislamu anayempwekesha Allah anatekeleza haki za mkewe, na anaogopea asimkosee Allah katika kutekeleza haki za mkewe na kumfanyia wema. amesema Allah Mtukufu: { Nao wanawake wanayo haki kwa sheria kufanyiwa na waume zao] kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao} [Al-baqarah :228]

Akasema Mtume[s.a.w]{Mbora wenu ni yule mbora kwa watu wake, nami nimbora wenu kwa watu wangu} [Imepokewa na Atirmedhi]

Na walipokuja wanawake wakiwashitaki waume zao kwa Mtume[s.a.w] akasema {Mbora wenu ni Yule mbora kwa wake zake} [Imepokewa na Ibn Majah]

 1. kuamiliana na mume

Tawheed inazalisha katika moyo wa mwanamke wakiislamu uchaji, ambao ni sababu kuu yakutekeleza haki za mumewe, ili umfikishe na kumuingiza peponi. amesema Mtume[s.a.w] «Atakaposali mwanamke sala zake tano, na akafunga mwezi wake wa Ramadhani, na akajistiri mwili wake, na akamtii mumewe, ataambiwa siku ya kiyama: ‘ingia peponi na mlango wowote anaotaka» (Imepokewa na Ahmad)

Na Allah akamkanya kutomkalifisha mumewe mambo asiyokuwa nayo uwezo, amesema Allah Mtukufu: { Mwenye wasaa agharimu kadiri ya wasaa wake; na yule ambaye amepungukiwa riziki yake, atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri ya alichompa. Atajaalia Mwenyezi Mungu baada ya dhiki faraji.} [At-talaaq : 7]

Asimuombe talaaqa bila sababu amesema Mtume [s.a.w]: «Mwanamke yeyote atayemuomba mumewe talaka bila ya sababu ni haramu kwake kupata harufu ya pepo» (Imepokewa na Ahmed)

KUAMILIANA NA JAMAA WA KARIBU NA

MAJIRANI

Kuunga udugu na haki za jirani

Allah alieka sawa baina ya kumuabudu yeye pekee kwa kumpwekesha yeye, na kuamiliana, na tabia nzuri ya kiislamu katika kuamiliana kwa muislamu na watu wake wakaribu na majirani zake; amesema Allah Mtukufu: { Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri,} [An nisaa : 36]

Amesema Mtukufu: { Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa.} [Ar-rum :38]

Akasema Mtume[s.a.w] «Anayemuamini Allah na siku ya mwisho, afanye wema kwa jirani yake»(Imepokewa na Muslim)

KUAMILIANA NA WATU KAZINI NA WATU WOTE:

Imani inaleta kwenye moyo wa muislamu mwenye kumpwekesha Allah tabia nzuri, kunasiihana, na kuamiliana kwa ukweli bila udanganyifu, haya ni baadhi ya matendo bora anayojikurubisha mja kwa Allah Mwenye nguvu na utukufu.

 1. tabia njema:

Amesema Allah kumsifu nabii wake [s.a.w] {Bila shaka una tabia njema kabisa.} [Qalam:4]

Akasema Mtume [s.a.w]

« jambo ambalo niwawaingiza watu peponi sana ni kumcha Allah na kuwa na tabia nzuri» (Imepokewa na Atirmidhi)

Akasema tena Mtume [s.a.w] «mtu anayependwa zaidi na Allah ni mtu mwenye manufaa kwa watu, na amali bora inayopendeza ni kumuingiza ndugu yako muislamu, ama kumuondoshea tatizo ama kumlipia deni” Ima kumuondoshea njaa, na hakika kuenda na ndugu yangu ili nimsaidie kukidhi haja zake ninapenda zaidi kuliko kufanya itikafu katika msikiti huu [yaani msikiti wa Madina] mwezi mmoja»
(Imepokewa na At-tabaran)

 1. Ukweli, amesema Allah Mtukufu: {Enyi mlioamini mcheni Allah kikweli kweli na muwe miongoni mwawasemao ukweli} [Attawbah: 119]

Akasema Mtume [s.a.w] «Hakika ya ukweli unaongoza kwa wema na wema unaongoza peponi, na mtu hataacha kusema ukweli mpaka awe mkweli, na hakika uongo unaongoza kwenye uovu na mtu haacha kusema uongo mpaka anaandikwa mbele ya Allah kuwa muongo»
(Imepokewa na Albukhari)

Akasema tena Mtume[s.a.w] «Aya na alama za mtu mnafiki ni tatu: akisema husema uongo, na akieka ahadi hukhalifu [hatimizi]na akiaminiwa hufanya khiyana» (Imepokewa na Albukhari)

 1. Nasaha na kutofanya udanganyifu, amesema Mtume [s.a.w] «Hakuna mja yeyote atakayepewa madaraka kisha afe siku ya kifo chake, na alikuwa mdanganyifu, ispokuwa Allah atamuharamishia pepo.» (imepokewa na muslim)

Alipita Mtume [s.a.w] siku moja sokoni akaona chakula chauzwa, akatia mkono wake ndani ya chakula akapatwa na unyevu wa chakula .akasema :«nini hii ewe mwenye chakula? Akasema : kimepatwa na mvua ewe Mtume wa Allah, akasema Mtume [s.a.w]: mbona usikieke juu ili mtu ajionee mwenyewe kabla hajanunua, mwenye kughushi simiongoni mwetu.»
(Imepokewa na Muslim)

Ni muhali kudhani kwamba Mtume [s.a.w] aliye fundisha umati wake jinsi ya kustanji [kutamba] kisha asiwafundishe kumpwekesha Allah, na tawhiid ndio aliosema Mtume [s.a.w]: «nimeamrishwa kupigana na watu paka washuhudie kuwa hakuna apaswaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah»
(imepokewa na Albukhari) kipi kilicho hifadhi mali na uhai wa watu ispokuwa uhakika wa tawhiid.

[Imam Maalik Ibn Anas]

Marejeo

 1. ni kipi kiwango cha lazima cha athari za ibada makhsusi katika mwenendo na vitendo hivi :

Tohara , Sala , Zaka , Saum ,Hajj,

 1. vipi atakuwa na imani asiye Sali? lete hoja kwa unayo yasema.
 2. je! Inawezikana mtu akasali kisha sala yake isimzuie na maovu na machafu?
 3. Utadhihirika vipi uhusiano wa kumuamini Allah na kuamiliana na watoto na mke na jamaa za karibu na jirani na watu wote?

MTAMBUE ALLAH KWA MAJINA YAKE NA SIFA ZAKE

{Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri; muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaoharibu utakatifu wa majina yake. Karibuni hivi watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda}.[al aaraf : 180]