Kuamini kukutana na Allah

Kuamini kukutana na Allah

Kuamini Kukutana Na Allah

Kila Kiumbe Kitarudi Kwa Allah Na Kwake Ndio Marejeo Ya Kila Kitu, Na Hii Ni Nguzo Muhimu Sana Katika Nguzo Za Imani, Miongoni Mwa Nguzo Za Imani Kuamini Siku Ya Mwisho Imethibiti Kuwa Mtume (S.A.W) Alipoulizwa Na Jibril (A, S) Mbele Ya Maswahaba Kutaka Kuwafundisha Nguzo Za Imani. Akasema. “Ni Kuamini Allah Na Malaika Wake Na Vitabu Vyake Na Mitume Wake Na Siku Ya Mwisho Na Kuamini Qadari Kheri Na Shari Yote Yatoka Kwa Allah.” (Imepokewa Na Muslim)

Na Imeitwa Siku Ya Mwisho Kwasababu Hakuna Siku Baada Yake Watakapo Kuwa Watu Wapeponi Peponi Na Watu WA Motoni Motoni. Na Iko Na Majina Mengi Katika Quran Tukufu Inayojulisha Utukufu Wake Na Ukubwa Wake Na Yatakayo Tokea Siku Hiyo:

Siku Ya Kutokea Jambo Kwasababu Siku Hiyo Itatokea , Na Khafidha Yenye Kutweza Na Kunyenyua Kwasababu Watanyenyuliwa Watu Darja Peponi Na Watatweza Wengine Motoni, Siku Ya Hisabu Na Malipo, Na Siku Ya Dini Na Siku Ya Haki Ambayo Khabari Zake Allah Zitakuwa Kweli, Siku Ya Balaa Na Siku Ya Sauti Kali Iumizayo Mashikio, Kwasababu Mpulizo Wa Baragumu Unaleta Uziwi, Na Siku Na Ahadi, Kwakutimia Ahadi Zake Allah Juu Ya Makafiri, Na Siku Ya Hasara, Kwa Hasara Na Majuto, Na Siku Ya Kukutana, Kwasababu Watu Wote Watakutana Sehemu Moja, Na Siku Iliyo Karibu Kwa Ukaribu Wake, Siku Ya Kuitana, Kwasababu Ya Watu Kuitana Watu Wa Peponi Watawaita Watu Wa Motoni Na Watu Wa Motoni Wawaite Watu Wa Peponi Na Siku Tasa Siku Ya Mwisho Hakuna Siku Baada Yake Na Nyumba Ya Mwisho Na Nyumba Ya Milele Na Siku Ya Kufinika Kwa Sababu Itafinika Watu Na Majina Mengine .

YANAYO AMBATANA NA IMANI YA SIKU YA MWISHO:-

MWanzo: KuamiNi ya baada ya mauti:

Kama Fitna Ya Kaburini : Nayo Ni Kuulizwa Maaiti Baada Yakuzikwa Kuhusu Mola Wake Na Dini Yake Na Nabiyi Wake, Hapo Huwathubutisha Allwah Kwa Neni La Kuthubutu Wale Ambao Wameamini, Akaseama: ( Mola Wangu Ni Allwah, Na Dini Yangu Ni Uislamu, Na Mtume Wangu Ni Muhammad), Na Huwapoteza Allwah Walio Madhalimu Hapo Husema Alio Kafiri:(Ha..Ha... Sijui), Na Husema Mnafiki Au Mwenye Shaka: (Sijui Nimesikia Watu Wakisema Kitu Nami Nikasema).

Na Miongoni Mwa Adhabu Za Kabri Na Neema Zake: Adhabu Ya Ya Kaburi Huwa Ni Yamadhalimu Na Manafiki Na Makafiri, Na Baadhi Ya Maasi Miongoni Ya Waumini.Amesema Allwah Mutukufu: {Na Lau Ungewaona Madhalimu Kwenye Matungu Ya Mauti Na Malaika Wamenyosha Mikono Yao Toeni Roho Zenu Leo Mtalipwa Adhabu Ya Utwevu Kwa Yale Mulikuwa Mukiyasema Kwa Mungu Yasiokuwa Ya Haki Na Mulikuwa Mukifanya Kibri Kwa Aaya Zake} (Al-An’am 93)

&"Alikuwa Uthman Akisimama Juu Ya Kaburini Hulia Mpaka Akarowesha Ndevu Zake Akasema: Akaambiwa: Kwatajwa Pepo Na Moto Hulii, Na Walia Kwa Hili? Kasema: Hakika Mtume WA Mwenyeezzi Mungu Alisema:” Hakika Kaburi Ni Mashukio Ya Kwanza Katika Mashukio Ya Akhera, Akiokoka Nayo Litkalo Kuja Baada Yake Ni Rahisi, Na Akitookaka Nayo Yaliyo Baada Yake Ni Magumu Zaidi” Akasema: Na Akasema: Sikuona Cha Kuangaliwa ILA Kaburi Yatisha Zaidi &"(Ameipokea Ahmed)

Allah Amesema Mtukufu Kuhusu Watu WA Firaun: {Watakuwa Wakionyeshwa Asubuhi Na Jioni Na Siku Itakapo Simama Kiyama (Kutaambiwa) Watiyeni Watu WA Firauni Kwenye Adhabu)} (Ghaafir 46)

Na Katika Hadith Ya Zaid Bin Thabit Kutoka Kwa Mtume ( S.A .W) “ Lau Kama Haingekuwa Hamtazikana , Ningemuomba Allwah Akawasikizisha Baadhai Ya Adhabu Ya Kaburi Ambayo Naisikia, Kisha Akatuelekea Kwa Uso Wake, Akasema : Twajilinda Kwa Mweneezzi Mungu Na Adhabu Ya Kaburi, Tukasema: Twajilinda Kwa Allwah Na Adhabu Ya Kaburi, Akasema: Twajilinda Kwa Allwah Na Adhabu Ya Kaburi, Tukasema: Twajilinda Kwa Allwah Na Adhabu Ya Kaburi, Akasema Twajilinda Kwa Allwah Na Fitna Zilizodhihiri Na Zilizojificha,Tukasema Twajilinda Kwa Allwah Na Fitna Zilizodhihiri Na Zilizojificha,Akasema Twajilinda Kwa Allwah Na Fitna Za Dajaali ” (Amepokea Muslim)

Ama Neema Za Kaburini Niza Waumini Wa Kweli, Amesema Allwah Mutkufu: { Hakika Wale Ambao Walisema Mola Wetu Ni Allwah Kisha Wakalingana Sawasawa Wanawateremkia Malaika (Kuwaambia) ,”Kwamba Musiche Wala Musihuzunike Na Furahikieni Pepo Ambayo Mlikuwa. } (Fusilat: 30)

Na Amesema Allah Mtukufu: {Basi Roho Itakapofika K’oni. Na Nyinyi Hapo Mwatizama .Nasi Tukokaribu Nayo Kuliko Nyinyi Lakini Hamuoni. Basi Laukama Hamutalipwa Mungeirudisha Hiyo Roho Ikisgafika K’oni Mungekuwa WA Kweli. Ama Akiwa Mwenye Kufa Ni Miongoni Waliokurubishwa Na Allwah. Atakuwa Na Raha Na Rizki Njema. Ama Akiwa Katika Watu WA Upande WA Kulia. Salama Ni Yako Kwakuwa Ni Katika Watu WA Kulia.Ama Akiwa Katika Wenye Kukanusha Walio Wapotevu.Basi Wana Mashukio Ya Moto WA Jahanam.Na Kuchomwa Katika Moto WA Jaihim.Hakika Huu Ndio Ukweli WA Yakini. Basi Litukuze Jina La Mola Wako Mtukufu} (Al-Waqiah 83- 96)

Na Amesema Kuhusu Mwenye Kuamini Akiwajibu Malaika Wa Wili Katika Kabri Yake &" Ataita Mwenye Kuita Kutoka Mbinguni Kwamba Amesema Kweli Mja Wangu, Mtandikieni Peponi,Na Mumvalishe Kutoka Peponi, Na Mumfungulie Mlango Wa Peponi, Akasema Hapo Yatamjilia Manukato Yake,Na Atafungulwa Kaburini Mwake Upeo Wa Macho Yake &" (Ahmed, Abu Dawud, Katika Hadeeth Ndefu)

Pili: kuamiNi kufufuliWa:

Nako Ni Kuwuhiyiwa Watu Kutakapo Viviwa Parapanda Viviwa La Pili, Watu Watasimama Kwa Ajili Ya Mola WA Viumbe Wote, Hali Yakuwa Bila Ya Viyatu, Wakiwa Uchi Bila Yakujisitiri, Wakiwa Mizunga Bila Yakutahiriwa, Amesema Allwah: {Kama Tulivoanza Kuumba Tutakuregesha Ni Ahadi Juu Yetu Hakika Sisi Ni Wenye Kulifanya Hilo)} (Al-Anbiyaaa 104)

Na Kufufuliwa Ni Haki Yenye Kuthubutu Ilio Onyeshwa Na Qur’an Na Sunnah Na Kongamano La Waislamu, Amesema Allwah Mtukufu: {Kisha Nyinyi Baada Ya Hapo Mutakufa. Kasha Nyinyi Siku Ya Kiyama Mutafufuliwa. } (Al-Mu’minun: 15-16)

Amesema Mtume (S.A.W) &" Watafufuliwa Watu Siku Ya Kiyama Bila Ya Viatu Na Mazunga &" (Mutafaqu Alaihi)

Na Wamekongamana Waislamu Kwa Kuthubutu Kwake, Na Hilo Ndilo La Hikma Linalotaka Mwenyeezzi Mungu Avaveke Hawa Viumbe Maregelewa Watakapolipwa Yale Waliolazimishwa Kwa Ndimi Za Mitume Wao. Amesema Allwah Mtukufu: {Mwadhania Kwamba Tumewaumba to Na Kwamba Hamutarudi Kwetu?} (Al-Muminun 115)

Na Mwenyeezzi Mungu Amewaambia Mitume: {Hakika Mwenyeezzi Mungu Ambae Amekufaradhia Qur’an Ni Mwenye Kukuregesha Kwenye Maregewa.!} (Al- Qasas 85)

Tatu: kuamiNi yaliyo kuja kuhusu alama Na ishara za siku ya kiyama:

Nazo Nizile Zitakazo Tangulia Kuja Kiyama Chenyewe Na Zenye Kuonyesha Ukaribu Wa Kuja Kwake, Na Kumezoewa Kuzigawanya Hizo Alama Mara Mbili Alama Za Ishara Ndogo Na Alama Za Ishara Kubwa.

Alama Ndogo : Nazo Nizenye Kutangulia Siku Ya Kiyama-Mara Nyingi- Kwa Muda Mrefu , Na Miongoni Mwazo Kuna Zilizitokea Na Zikamalizika- Na Henda Zikakaririka – (Kuja Mara Kwa Mara) Na Kuna Zilizo Jitokeza Na Zikaendelea Kujitokeza , Na Kuna Ambazo Hazijatoka Mpaka Sasa, Lakini Zitatoka Kama Alivosema Mkweli Mwenye Kusadikiwa-, Kama: Kutumilizwa Mtume Na Kufa Kwake, Na Kufunguliwa Betul-Makdisi,Na Kudhihiri Fitna, Na Kupotea Uwaminifu, Na Kupotea Ilmu Na Kudhihiri Ujinga, Na Kuenea Zina Na Riba, Na Kudhihiri Aala Za Nyimbo, Na Kuzidi Kunywewa Mvinyo, Na Kutukuka Wachunga Mbuzi Kwenye Majumba, Na Kuzidi Kuteta Watoto Na Wazazi Wao Mpaka Wajifanye Kama Kwamba Wao Ni Mabawana Zao, Na Kuzidi Kuwa Na Mitetemeko Ya Ardhi, Na Kudhihiri Kudidimizwa Na Kugeuzwa Na Kutukananwa, Na Kudhihiri Wanawake Walio Vaa Wenye Kuenda Uchi, Na Kuengezeka Kutolewa Ushahidi Wa Urongo Na Kufichwa Ushahidi Wa Ukweli, Na Mengi Yasio Kuwa Hayo Miongoni Yalio Kuja Katika Kitabu Cha Allwah Na Sunna Za Mtume.

Alama Kubwa : Nazo Ni Mambo Makubwa Kutaonyesha Kuja Kwayo Kukurubia Kuja Kiyama Na Kubaki Mda Mfupi Wa Kuja Hiyo Siku Kubwa, Nazo Ni Alama Kumi: Djali, Na Kuteremka Iysaa Mwana Wa Mariyamu, Na Yajuja Na Majuja, Na Kupatwa Mwezi Mara Tatu: Kupatwa Mashariki, Na Kupatwa Magharibi, Na Kupatwa Kwenye Kisiwa Cha Kiarabu, Na Moshi, Na Kutoka Jua Magharibi, Na Mnyama, Na Moto Ambao Utawapeleka Wato Kwenye Kufufuliwa Kwao, Na Alama Hizi Zitatokeza Kwa Kufuatana, Ikidhihiri Ya Kwanza Ya Pili Ya Fuatia.

NNE: kuamiNi yaliyo kuja kuhusu vituko vya kiyama Na matukio yake Kama:

1-Kusagwasagwa Majabali Na Kufanywa Mchanga Yawe Sawa Na Ardhi:

Amesema Allah Mtukufu {Na Utayaona Majabali Utayadhania Yametulia Nayo Yakimbia Yanavo Kimbia Mawingu.} (An-Namli 88)

Na Akasema Allah Mtukufu {Na Yatavunjwavunjwa Majabali Yawe Vumbi Lilo T’atawanywa} (Waqiah Aya 6-7)

Amesema Allah Mtukufu {Na Milima Itakuwa Kama Sufi (Inayoruka)} (Ma, Arij Aya 9)

Na Amesema Allah Mtukufu: {Na Wanakuuliza Kuhusu Majabali Sema Atayavunjavunja Allwah Kabisa. Atayawacha Kiwanda Kilicho Tandikwa. Hayana Uchini WA Ukubwa. } (Ta Ha Aya 105-107)

2-Kulepuka Bahari Na Kutiwa Moto, Hizi Bahari Zenye Kufinika Sehemu Nyingi Ya Ardhi Yetu, Zitalepuliwa Siku Hiyo, Amesema Allwah Mtukufu: {Nabahari Zitakapolipuliwa} (Infitar Aya 3) {Na Bahari Zitakapowashwa Moto} (Takwiyr Aya 6)

3-Kubadilika Ardhi Hii Wanayo Ijuwa Watu, Na Vilevile Mbingu, Wafufuliwe Juu Ya Ardhi Wasioijuwa, Amesema Allwah Mtukufu {(Siku Itakapobadilishwa Ardhi Iwe Sio Hii Ardhi Na Zibadilishwe Mbingu Na Watokeze Kwa Mwenyeezzi Mungu M’moja Mwenye Kushinda Nguvu.} (Ibrahim Aya 48)

Akasema Mtume (S.A.W) “Watafufuliwa Watu Siku Ya Kiyama Juu Ya Ardhi Nyeupe Yenye Kupigia Wek’undu Kama Donge La Unga Haina Alama Ya Yoyote &" (Mutafakun Alyhi), Itakuwa Nyeupe Bila Alama Yoyote.

4-Wataona Watu Wasilokulizowea Kwani Wataona Kukutana Jua Na Mwezi, Roho Zitazidi Kukereka Na Kubabaika, Amesema Allah Mtukufu {(Itakapo Duwala Jicho. Na Mwezi Ukazima Mwangaza Wake. Na Kukakusanywa Jua Na Mwezi. Atasema Mwanadamu Siku Hiyo Pakukimbilia Ni Wapi?} (Qiyamah Aya 7:10)

5-Kupulizwa Parapanda Na Ndiko Kukoma Maisha Haya Ya Ulimwenguni, Itakapokuja Siku Hiyo Kutapulizwa Parapanda, Kupulizwa Huku Kutakomesha Maisha Haya Ya Ulimwenguni. {Na Kutapulizwa Parapanda (Baragumu) Wasusuwikwe Walio Mbinguni Na Ardhini ILA Alio Wataka Mwenyeezzi Mungu (Wasiwe Hivo)} (Az-Zumar Aya 68)

Nako Ni Kupulizwa Kukubwa Kwenye Kuharibu Kila Kitu, Atakakokukusikia Mtu Na Asiweze Kufanya Lolote, Nawala Asiweze Kurudi Kwa Watu Wake Na Marafaki Wake : { Hawangojei Ila Ukelele Mmoja Tu Utakao Kuwashika Kwenye Hali Yakuwa Wanagombana . Hawatoweza Kutoa Wasia Nawala Hawatorudi Kwa Watu Wao} (Ya-Sin Aya 49-50)

Asema Mtume (S.A.W) { Kisha Kutapulizwa Baragumu Hatulisikia Yoyote Ila Ataipendua Na Ainue Shingo Yake, Akasema- (Mtume)Na Wakwanza Kusikia Hayo Ni Mtu Atakaekuwa Analitengeza Birika La Ngamia Wake,Akasema(Mtume) Atasusuwikwa(Kuanguka Na Kupoteza Fahamu)Na Watasusuwikwa Watu . } (Imepokewa Na Muslim)

6-Kufufuliwa Na Kukusanywa Kwa Viumbe Wote Tangu Alipo Viumba Allah Paka Siku Ya Kukusanywa, Watakusanyika Katika Uwanja Huo Tangu Wamwanzo Wao Mpaka Wamwisho Wao Majini Na Watu, Pia Wanyama, Amesema Allah: {Kwa Yakini Katika Haya Kuna Mazingatio Kwa Yule Anayeogopa Adhabu Ya Akhera.Hiyo Ndiyo Siku Itakayokusanyiwa Watu, Na Hiyo Ndiyo Siku Itakayo Shuhudiwa (Na Viumbe Wote)} (HUD Aya 103)

Asema Allah Mtukufu: {Sema, “Bila Shaka WA Kwanza Na WA Mwisho” “Watakusanywa Kwa Wakati (Uliowekwa) Katika Siku Maalumu.} (Waqiah 49:50)

7-Hakika Watu Watafufuliwa Wakiwa Uchi Kama Walivyo Umbwa Na Allah Wala Hawatapepesa Kushughulika Na Hilo Kwasababu Ya Ugumu Wa Sehemu Hiyo Na Kisimamo Hicho Chenye Kutisha, Hapo Alishangaa Mama Aisha (R.A) Akasema Kama Anavyo Simulia Mwenyewe ” Alisema Mtume Wa Allah (Mtafufuliwa Hali Mkiwa Uchi Hamja Tahiriwa),Akasema Aisha (R.A) Nikasema Ewe Mtume Wa Allah Wanaume Kwa Wanawake Wakiangaliana? Akasema Jambo Ni Gumu Zaidi Kuliko Kushughulika Na Hayo” (Imepokewa Na Bukhari)

8-Kulipiza Kisasi Kwa Mwenye Kudhulumiwa Hata Wanyama Nao Watalipizana Visasi Asema Mtume WA Allah (S.A.W): &" Hakika Mtarudisha Haki Zawatu Siku Ya Kiama Paka Ataletwa Mbuzi Asiye Na Pembe Amlipize Aliye Nazo Ambaye Alimdunga Duniani.&" (Imepokewa Na Muslim)

Na Akasema Tena (S.A.W) “Ambaye Alimdhulumu Nduguye Muislamu Kwa Cheo Chake Au Kwa Kitu Chochote Basi Ajivue Nacho Hapa Ulimwenguni Kabla Ya Siku Ya Kiama Ambapo Hazitafaa Pesa Bali Kama Ana Vitendo Vizuri Vitachukuliwa Kulingana Na Madeni Anayo Daiwa Na Kama Hana Vitendo Vyema Yatachukuliwa Maovu Ya Wenye Kudai Na Arundukiziwa Yeye .” (Imepokewa Na Bukhari)

9-Jua Kushuka Karibu Na Watu, Mpaka Watu Wafinikwe Na Majasho Yao Kulingana Na Vitendo Vyao Amesema Mtume Wa Allah (S.A.W) “Jua Litashushwa Karibu Siku Ya Kiama Mpaka Liwe Karibu Na Viumbe Kadri Ya Mail Moja, Akasema Suleim Bin Amri: ” Naapa Kwa Allah Sijui Alikusudia Nini Mail Moja? Sijui Ni Masafa Ya Ardhi Au Ni Kijiti Cha Kupakia Wanja? Akasema Watu Watakuwa Katika Majasho Yao Kadri Ya Matendo Yao, Kunaye Ambaye Jasho Litafika Visiginoni Mwao Na Kunao Yatafika Magotini Mwao Na Kunao Yatafika Shingoni Mwao Na Kunao Yatawafinika Majasho Yao Akaashiria Mtume (S.A.W) Kwa Mkono Wake Mdomoni Mwake.” (Imepokewa Na Muslim)

10-Kunaye Atachukua Kitabu Chake Kwa Mkono Wa Kulia, Na Kunaye Atachukua Kwa Mkono Wa Kushoto Kisha Watu Watakuwa Na Wasiwasi Na Uoga Paka Daftari Lake Liwe Mkononi Mwake Hapo Ndio Muumin Atafurahi Kwakuridhia Kufaulu Pindi Atakapo Shika Daftari Lake, Ilhali Makafiri Na Wanafiki Wanaongezeka Majonzi Na Wasiwasi Pindi Watapo Yakamata Madaftari Yao Kwa Mikono Yao Ya Kushoto, Hayo Ni Malipo Yaliyo Sawa,Asema Allah Mtukufu : { Basi Ama Yule Atakayepewa Daftari Lake Kwa Mkono Wake Wa Kiume (Kulia) Atasema (Kwa Faraha)” Haya Someni Daftari Langu (Nililopewa Sasa Hivi). ”Hakika Nilijua Ya Kuwa Nitapokea Hisabu Yangu (Kwa Vizuri, Kwani Nikifanya Mazuri)” Basi Yeye Atakuwa Katika Maisha Ya Raha .Katika Pepo Tukufu. Vishada Vya Matunda Yake Vitakuwa Karibu ;( Vinachumika Bila Ya Taabu) (Waambiwe): Kuleni Na Mnywe Kwa Furaha Kwa Sababu Ya Vitendo Mlivyofanya Katika Siku Zilizopita. ”Walakini Atakayepewa Daftari Lake Kwa Mkono Wake Wa Kushoto Basi Yeye Atasema.”Ooh Laiti Nisingalipewa Daftari Langu.”Wala Nisingalijua Ninini Hisabu Yangu.” Laiti (Mauti) Yangemaliza (Kila Kitu Changu)”Mali Yangu Haikunifaa.”Usultani (Ukubwa) Wangu Umenipotea. } (Alhaqqah 19-29)

11-Yatayomsibu Mtu Katika Hofu Na Uoga Kiwango Mtu Hawezi Kumuuliza Mwingine Lolote Halimshughulishi ILA Nafsi Yake Anasema Allah Mtukufu: {Siku Ambayo Hayatafaa Mali Wala Watoto} (Ash-Shuaraa 88)

Naakasema Allah Mtukufu {Siku Ambayo Mtu Atamkimbia Nduguye. Na Mamaye Na Babaye. Na Mkewe Na Wanawe.Kila Mtu Miongoni Mwao Siku Hiyo Atakuwa Na Hali Itakayomtosha Mwenyewe, (Hana Haja Ya Mwenziwe)} (Abasa Aya 34-37)

TANO: kuamiNi hisabu Na malipo:

Mwanadamu Yatahesabiwa Matendo Yake Kishaalipwe Kulingana Na Matendo Yake, Asema Allah Mtukufu: {Hakika Marejeo Yao Ni Kwetu. Kisha, Bila Shaka, Hisabu Yao Ni Juu Yetu. } (Al-Ghashiyah Aya 25:26)

Asema Allah Mtukufu: {Afanyaye Kitendo Kizuri, Atalipwa Mfano Wake Mara Kumi. Na Afanyaye Kitendo Kibaya Hatalipwa ILA Sawa Nacho Tu (Basi, Kwa Rehema Ya Mwenyezi Mungu). Nao (Wote Hao) Hawatadhulumiwa.} (Al An-Am 160)

Na Akasema Allah Mtukufu: { Nasi Tutaweka Mizani Za Uadilifu Siku Ya Kiama,Na Nafsi Yoyote Haitadhulumiwa Hata Kidogo.Na Hata Kama Likiwa(Jambo Hilo Lina )Uzito Mdogo Wa Chembe Ya Hardali Nalo Tutalileta;Nasi Tunatosha Kuwa Wajuzi(Wazuri Kabisa)Wa Hesabu. } (Al-Anbiyaa Aya 47)

Na Imepokewa Na Ibn Umar (R.A.A) Kutoka Kwa Mtume Wa Allah “Hakika Allah Atamsongelea Muumin Siku Ya Kiama Amfunike Kisha Amuulize Walikumbukaa Dhambi Lako Fulani Aseme Muumin Ndio Ya Allah Mola Wangu Mpaka Akiyakiri Madhambi Yake Akidhani Ameshaangamia Atasema Allah Nimekusitiri Duniani Na Leo Nakusamehe Kisha Atapewa Daftari Lake La Matendo Mema, Ama Makafiri Na Wanafiki Wataitwa Mbele Ya Viumbe,{Hao Ndio Walimzulia Mola Wao Uwongo” Sikizeni Laana Ya Mwenyezi Mungu Iko Juu Ya Madhalimu.}(HUD Aya 18) &"(Mutafakun Alyhi)

Na Imeswihi Kutoka Kwa Mtume (S.A.W.) Kwa Hadith Aliyo Ipokeya Kutoka Kwa Mola Wake Mtukufu Amesema: “ Hakika Allah Ameandika Mema Na Mabaya Kisha Akayapambanua Basi Mwenye Kuazimia Kutenda Jema Kisha Asilifanye Allah Humuandikia Jema Kamili Na Anapo Azimia Kutenda Jema Kisha Akalifanya Allah Humuandikia Mema Kumi Na Humuongezea Hadi Elfu Sabiin Na Mara Nyingi Zaidi , Ma Mwenye Kuazimia Kutenda Baya Moja Kisha Asilifanye Allah Humuandikia Jema Kamili Na Anapo Azimia Baya Kisha Aklifanya Allah Humuandikia Baya Moja ” (Mutafakun Alyhi)

Wameafikiana Waislamu Wote Kuwepo Kuhesabiwa Na Kulipwa Kulingana Na Matendo, Na Jambo Hili Liniwafiki Akili Kwa Sababu Allah Aliteremsha Vitabu Na Akatuma Mitume, Na Akafaradhishia Watu Kumuamini Na Kumtii Yeye, Kisha Akakhofisha Mwenye Kuacha Kumtii Na Kutomuamini Na Kutowatii Mitume Yake Kwa Adhabu Kali Na Yenye Kuumiza Siku Ya Kiyama Kama Kusingekuwa Na Hisabu Wala Malipo Yangalikuwa Haya Yote Ni Upuzi Ambao Allah Hasifiki Kufanya Jambo La Ki Puzi Lisilokuwa Na Faida. Ameashiria Allah Kwahilo Aliposema: {Na Kwa Yakini Tutawauliza Wale Waliopelekewa (Mitume), Na Pia Tutawauliza (Mitume) Waliopelekwa. Tena Tutawaambia Kwa Ujuzi (Uliokamili Kila Walilolitenda) Wala Hatukuwa Mbali (Nao Walipokuwa Wakifanya)} (Al-Aaraf 6:7)

SABA: KUAMINI PEPO NA MOTO :

Aliulizwa Hassan Basri Mbonaa Twaona Mataabiin Wanafanya Ibada Sana Kuliko Maswahaba, Kwa Jambo Gani Maswahaba Waliwatangulia? Akasema Hassan Hawa Wanafanya Ibada Lakini Dunia Iko Moyoni Mwao Lakini Maswahaba Walifanya Ibada Ikiwa Akhera Iko Moyoni Mwao.

Kwamba Ni Marudio Ya Milele Kwa Viumbe , Pepo Ni Nyumba Ya Neema Alizoziandaa Allah Kwa Waumini Wenye Kumcha Yeye, Walioamini Waliyofaradhishiwa Na Allah Na Wakamtii Allah Na Mtume Wake Kwa Kumtakasia Yeye Peke Yake Ibada, Wakimfuata Mtume Wake, Kuna Aina Za Neema Zote Ambazo Hakuna Jicho Lililowahi Kuziona Wala Hakuna Sikio Lililowahi Kuzisikia Wala Hakuna Mtu Aliyefikiria Hizo Neema. Asema Allah Mtukufu: {Hakika Wale Walioamini Na Kutenda Mema, Basi Hao Ndio Wema WA Viumbe. Malipo Yaokwa Mola Wao Nimabustani Ya Daima Ambayomito Inapita Mbele Yake, Wakae Humo Milele; Mwenyezi Mungu Amewaridhia, Nao Wameridhika (Malipo) Hayo Ni Kwa Yule Anayemuogopa Mola Wake} (Al-Bayyinah 7:8)

Akasema Tena Allah Mtukufu: {Nafsi Yoyote Haijui Waliyofichiwa Katika Hayo Yanayofurahisha Macho (Huko Peponi): Ni Malipo Ya Yale Waliyokuwa Wakiyafanya} (As-Sajdah Aya 17)

Na Neema Bora Zaidi Kuliko Zote Nikumtazama Allah Mtukufu Huko Peponi. Amesema Allah Mtukufu: {Nyuso (Nyingine) Siku Hiyo Zitangara (Kweli Kweli).Zinamtazama Mola Wao (Au Neema Alizo Wapa)} (Al-Qiyama Aya 22-23)

Amesema Allah Mtukufu: {Wale Waliofanya Wema Watapata (Jaza Ya) Wema (Wao) Na Zaidi} (Yunus 26)

Wema Uliotajwa Hapa Ni Pepo Na Zaidi Iliotajwa Hapa Ni Kumuangalia Allah Mkarimu Kama Alivyo Sema Mtume (S.A.W) “Watakapo Ingia Watu WA Peponi Peponi Mwao Atasema Allah Mtukufu: Je Mwataka Kitu Chochote Ni Waongezee? Watasema Kwani Hujazifanya Nyuso Zetu Tiyari Nyeupe Kwani Si Umetuingiza Tayari Peponi Na Ukatuepusha Na Moto, Akasema Hapo Ndipo Itafunguliwa Pazia, (Na Wamuone Allah) Basi Hakuna Kitu Bora Walichokitaka Kama Kumuona Allah Mtukufu Kisha Akasoma Mtume (S.A.W) Aya Hii: { Wale Walifanya Wema Watapata (Jaza Ya) Wema (Wao)Na Zaidi }(Yunus 26) &" (Imepokewa Na Muslim)

Ama Moto Ni Nyumba Ya Adabu Aliyoiandaa Allah Mtukufu Kwa Makafiri Na Wanafiki Madhalimu Waliomkufuru Yeye Na Wakawakanusha Mitume, Ndani Humo Mna Aina Zote Adabu Na Majonzi Wasiyoweza Kufikiriiwa. Asema Allah Mtukufu: {Na Ogopeni Moto Ambao Umewekewa Wenye Kukanusha Amri Za Mwenyezi Mungu} (Aali Imran Aya 131)

Akasema Tena {Hakika Tumewaandalia (Tumewawekea Tayari) Madhalimu Moto Ambao Kuta Zake Zitawazunguka. Na Wakiomba Msaada (Kwa Kiu Kubwa Iliyowashika) Watasaidiwa Kwa Kupewa Maji Kama Shaba Iliyoyayushwa Itakayoziunguza Nyuso Zao. Kinywaji Kibaya Kilioje Hicho. Na Mahali Pabaya Palioje. } (Al Kahf Aya 29)

Asema Allah Mtukufu: {Kwahakika Mwenyezi Mungu Amewalaani Makafiri Na Amewaandalia Moto Unaowaka Kwelikweli. Watakaa Humo Daima; Hawatapata Kipenzi Wala Msaidizi. Siku Ambayo Nyuso Zao Zitapinduliwa Pinduliwa (Zitapounguzwa) Motoni, Waseme:” Laiti Tungemtii Mwenyezi Mungu Na Tunge Mtii Mtume. } (Al-Ahzab Aya 64-66)

Yule Ambaye Atapata Adhabu Duni Zaidi, Allah Atuepushe Ni Kama Alivyo Msifia Mtume (S.A.W): “Hakika Mtu Atakaye Kuwa Na Adabu Duni Motoni Siku Ya Kiama, Ni Mtu Ambaye Ataekewa Kaa La Moto Katika Nyayo Yake Lakini Ubongo Wake Utachemka.&" (Imepokewa Na Bukhari)

MATUNDA YA KUAMINI SIKU YA MWISHO:

1-Ni Kuhakikisha Nguzo Moja Katika Nguzo Za Imani Kwasababu Kumuamini Allah Hakuwi Sawa Paka Mtu Aamini Siku Ya Mwisho Kwahiyo Ni Miongoni Mwa Nguzo Za Imani Ndio Maana Allah Alitufaradhishia Sisi Kumpiga Asiyeamini Hiyo Siku Ya Mwisho. Akasema Allah Mtukufu: {Piganani Na Wale Wasiomuamini Mwenyezi Mungu Wala Siku Ya Mwisho} (At Tawba 29)

2-Kupata Utulivu Duniani Na Akhera Na Ahadi Ya Malipo Makubwa, Asema Allah Mtukufu: {Sikizeni Vipenzi Vya Mwenyezi Mungu Hawatakuwa Na Khofu (Siku Ya Kiyama) Wala Hawatahuzunika} (Yunus 62)

3-Ahadi Ya Malipo Makubwa, Asema Allah Mtukufu: {Katika Walioamini (Mitume Ya Zamani Huko) Na Mayahudi Na Wakristo Na Wasabai; Yoyote (Miongoni Mwao) Atakayemwamini Mwenyezi Mungu (Sasa Kama Anavyosema Nabii Muhammad) Na Akaamini Siku Ya Mwisho Na Akafanya Vitendo Vizuri, Basi Watapata Thawabu Zao Kwa Mola Wao, Wala Haitakuwa Khofu Juu Yao, Wala Hawatahuzunika} (Al Baqarah 62)

4-Kuhimiza Katika Kufanya Vitendo Vizuri, Asema Allah Mtukufu: {Enyi Mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu Na Mtiini Mtume Na Wenye Mamlaka Juu Yenu, Walio Katika Nyie (Waislamu Wenzenu). Na Kama Mkikhitilafiana Juu Ya Jambo Lolote Basi Lirudisheni Kwa Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake, Ikiwa Mnamwamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho Hiyo Ndio Kheri, Nayo Ina Matokeo Bora Kabisa. } (A Nisaa Aya 59)

Na Akasema Allah Mtukufu: {Wanaoimarisha Misikti Ya Mwenyezi Mungu Ni Wale Wanaomuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho} (At Tawba 18)

Na Asema Allah Mtukufu: {Bila Shaka Mnao Mfano Mwema (Ruwaza Nzuri) Kwa Mtume WA Mwenyezi Mungu, Kwa Mwenye Kumuogopa Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho, Na Kumtaja Mwenyezi Mungu Sana.} (Al-Ahzab 21)

Na Akasema Allah Mtukufu {Kwa Yakini Umekuwa Mfano Mzuri Kwenu Katika Mwendo Wao, Kwa Amuogopaye Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho.} (Al-Mumtahinah 6)

Asema Allah {Na Simamisheni Ushahidi Kwa Ajili Ya Mwenyezi Mungu. Hivyo Ndivyo Anavyoagizwa Yule Anayemuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho. } (At-Talaq 2)

Amesema Alhasan (R.A):” Mwenye Kuyatambua Mauti Yanakuwa Masaibu Ya Dunia Yote Kwake Dhalili.

5-Anakataza Kutenda Vitendo Vibaya: Amesema Allah Mtukufu: {Wala Haiwajuzii Kuficha (Mimba) Aliyoumba Mwenyezi Mungu Katika Matumbo Yao, Ikiwa Wanamwamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho.} (Al-Baqarah 228)

Na Asema Allah Mtukufu: {Na Mtakapowapa Wanawake Talaka, (Ya Kwanza Au Ya Pili); Nao Wakamaliza Eda Yao, Basi (Nyinyi Jamaa WA Mke) Msiwazuie Kuolewa (Au Kurejewa) Na Waume Zao Endapo Baina Yao Wamepatana. Hayo Anaonywa Nayo Yule Miongoni Mwenu Anayemwamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho.} (Al-Baqarah 232)

Amesema Allah Mtukufu: {Hawatakuomba Ruhusa Wale Wanaomuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho. (Hawatakutaka Ruhusa) Kutoipigania Dini Ya Mwenyezi Mungu Kwa Mali Zao Na Nafasi Zao. Na Mwenyezi Mungu Anawajua Wanaomcha. Wanakuomba Ruhusa Wale Wasiomuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho, Na Nyoyo Zao Zina Shaka; Kwa Hiyo Wanasitasita Kwa Ajili Ya Shaka Yao.} (At Tawba: 44, 45)

Kwahio Asiyeamini Siku Hii Hajichungi Na Kufanya Yaliyo Haramishwa, Wala Haoni Haya Kwa Allah: {Je Umemuona (Unamjua) Yule Anayekadhibisha Dini, (Asiyeamini Malipo Ya Akhera)? Huyo Ni Yule Anayemsukuma Yatima. Wala Hajihimizi Kuwalisha Maskini (Wala Hawahimizi Wenziwe)} (Maun 1:3)

6-Kuwaliwaza Waumini Kwa Yanayo Mpita Hapa Duniani Kwa Neema Na Thawabu Anazo Zitarajia Kesho Akhera, Kwani Pepo Ndio Kufaulu Kukubwa Na Hayawi Maisha Ya Dunia ILA Starehe Zenye Kudanganya. Asema Allah Mtukufu: {Kila Nafsi Itaonja Mauti. Na Bila Shaka Mtapewa Ujira Wenu Kamili Siku Ya Kiyama. Na Aliyewekwa Mbali Na Moto Na Akaingizwa Peponi, Basi Amefuzu (Amefaulu Kweli Kweli). Namaisha Ya Dunia (Hii) Si Kitu ILA Ni Starehe Idanganyayo (Watu)} (Aa-Li Imran 185)

Moyo Hauwi Sawa Wala Hautengei, Wala Haupati Raha Wala Hautulii Na Kupata Utulivu ILA Kwa Kumuabudu Mola Wake Na Kumpenda Na Kurudi Kwake.

Sheikh Al Islam

Amesema Allah Mtukufu: {Sema: &" Mimi Naogopa Adhabu Ya Siku Kubwa (Hiyo) Ikiwa Nitamuasi Mola Wangu.” Atakaye Epushwa Nayo (Adhabu Hiyo) Siku Hiyo (Ya Kiyama), Bila Shaka Amemrehemu (Mwenyezi Mungu); Na Huku Ndiko Kufaulu Kuliko Dhahiri.} (Al An-Am: 15:16)

Na Akasema Allah Mtukufu: {Hali Ya Kuwa Ya Akhera Ni Bora (Zaidi Kabisa) Na Yenye Kudumu.} (Al-Ala A: 14)

Kumliwaza Muumini Kwa Yale Yanampita Duniani. Kwa Zile Neema Na Thawabu Anazo Zisubiri Muumin, Kwa Hiyo Pepo Ni Kufaulu Kukubwa Sana, Na Hayakuwa Maisha Yaa Duniani ILA Starehe Yenyekuhadaa. Asema Allah Mtukufu. {Kila Nafsi Itaonja Mauti. Na Bila Ya Shaka Mtapewa Ujira Wenu Kaamili Siku Ya Kiyama. Na Atakaye Epushwa Na Moto Na Akatiwa Peponi Basi Huyo Amefuzu. Na Maisha Ya Dunia Si Kitu ILA Ni Starehe Ya Udanganyifu. } (Aa-Li Imran 185)

Asema Allah Mtukufu: {Sema: “Mimi Naogopa Adhabu Ya Siku Kubwa (Hiyo) Ikiwa Nitamuasi Mola Wangu.” Atakaye Epushwa Nayo (Adhabu Hiyo) Siku Hiyo (Ya Kiyama), Bila Shaka Amemrehemu (Mwenyezi Mungu); Na Huku Ndiko Kufaulu Kuliko Dhahiri} (Al An-Am: 15:16)

Asema Allah Mtukufu {Hali Ya Kuwa Ya Akhera Ni Bora (Zaidi Kabisa) Na Yenye Kudumu.} (Al-Alaa: 14)



Tags: