Kumpenda Allah

Kumpenda Allah

Maana ya kumpenda Allah:

Kumpenda Allah

Ni liwaza ya moyo kwa kuegemea kwa Allah, na kutii yote ayatakayo Allah, na jina la Allah litawale na kustawi katika moyo.

Uhakika wa kumpenda Allah

Kumpenda Allah ni kupenda ibada zake, na kujidhalilisha kwake, na kumtukuza yeye, na uwe moyo wa mwenye kumpenda ni wenye kumtukuza Allah kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake, na mapenzi haya ndio asili ya imani na uhalisi wa tawhiid, na zinaambatana nayo fadhila nyingi ambazo hazihesabiki, na miongoni mwa kumpenda Allah ni kupenda anavyopenda Allah miongoni mwa sehemu, nyakati, watu na vitendo na maneno, na mengineyo anayoyapenda Allah.

Kama vile kumpenda Allah kunatakiwa kuwe kwa kikweli kweli kwake pekee, na hii haiendi kinyume na mapenzi ya kawaida, kama mtoto kumpenda babake na baba kumpenda mwanawe na mwanafunzi kumpenda mwalimu wake au kupenda chakula flani na kinywaji flani na kupenda kuoa au kuvaa au kupenda marafiki na mengineo.

Ama mapenzi yaliyo haramishwa nayo ni kama ushirikina katika kumpenda Allah, kama washirikina wanavyo yapenda masanamu yao na kuwapenda vipenzi wao washirikina, ama kutanguliza matamanio ya nafsi kuliko anayoyapenda Allah, au kupenda asivyo vipenda Allah katika nyakati au sehemu au watu au vitendo au maneno, navyo vitu hivi viko tabaka tabaka, amesema Allah Mtukufu: {Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana}
[Al baqarah : 165]

Miongoni mwa fadhila za kumpenda Allah 

 

 1. Ni msingi wa tawhiid, na roho yake nikumtakasia mahaba Allah pekee, bali hii ndiyo uhakika wa ibada, na haikamiliki tawhiid mpaka yakamilike mapenzi ya mja kwa Mola wake na yatangulie mapenzi ya kila kitu na yayashinde, na yawe ndiyo yanaamrisha, mpaka awe mtu kupenda kwake kunaenda kulingana na mapenzi haya. Mapenzi ambayo ndani yake muna furaha ya mja na kufaulu kwake.
 2. Kuliwazwa mwenye kupenda wakati wa matatizo na misukosuko, kwahiyo mwenye kupenda anapata ladha na utamu wa mapenzi unao msahulisha misiba na matatizo, na mambo mazito kwake yanakuwa mepesi.

Hajaabudiwa Allah kwa ibada nzuri kuliko ibada iliokusanya mapenzi yake, kuogopa adhabu zake na kutaraji rehema zake.

Kuwa na shauku ya kukutana na Allah na kukutana na upepo mzuri ambao utapulizwa moyoni ili uondoe mafundo ya dunia.

 1. Ukamilifu wa neema na mwisho wa furaha: na haya hayawezifikiwa isipokuwa kwa kumpenda Allah Mtukufu, moyo hautosheki wala haufikii matakwa yake wala haushibi ispokuwa kwa kumpenda Allah na kuelekea kwake, na hata kama mja atapata kila kinacho mletea raha na utamu na kumliwaza, lakini hawezi kupata utulivu wala raha na starehe ila kwa kumpenda Allah, kwa hiyo kumpenda Allah ndio neema ya kipekee ya nafsi, hakuna kwa wenye na akili timamu na nyoyo nzima, kitu chochote kitamu wala kizuri wala chenye kufurahisha wala chenye neema kuliko mapenzi ya Allah na riwaza zake na shauku ya kutaka kukutana naye. Na utamu anaoupata muumini moyoni mwake unashinda utamu wa kila kitu , na neema ambazo anazipata ni neema zilizo kamilika kuliko neema zozote, na ladha anayoipata iko juu kuliko ladha yoyote nyengine. «Mambo matatu mwenye kuwa nayo amepata utamu wa imani : awe Allah na Mtume wake ni vipenzi vyake zaidi kuliko chochote, na akimpenda mtu ampende kwa ajili ya Allah , na achukie kurudi kwenye ukafiri baada ya kutolewa huko kama vile anavyochukia kutupwa ndani ya moto»
  (Imepokewa na Bukhari na Muslim na An-nasaai)

Ni ubaya ulioje kwa mtu aliyenyimwa utulivu na raha kutoka kwa Allah. 

 

SABABU ZA KULETA MAPENZI YA ALLAH 

 

Mola wetu Mkarimu anampenda ampendae na mwenye kujikurubisha kwake, na sababu ya kwanza inayoleta mapenzi ya Allah, ni mja kumpenda Mola wake, na maelezo zaidi ya sababu za kuleta mapenzi ya Allah ni kama ifuatavyo:

 1. kusoma quran kwa kuzingatia na kufahamu maana yake na yaliyo kusudiwa, basi mwenye kujishughulisha na kitabu cha Allah na kutenda kulingana nacho basi moyo wake utaimarishwa na mapenzi ya Allah.
 2. kujikurubisha kwa Allah kwa kufanya vitu vya nafli [vya suna] baada ya faradhi «Na hataacha mja wangu kujikaribisha kwangu kwa vitendo vya suna mpaka ni mpende, na nitakapompenda nitakuwa kama sikio lake lakusikizia au jicho lake lakuonea au mkono wake wakushikia au mguu wake wakutembelea, na atakapo niomba chochote nitampa na akiniomba msaada nitamsaidia.»(Kutoka kwa Qais imepokea na Bukhari)
 3. kudumu kumtaja Allah katika kila hali, kwa ulimi au moyo au kwa vitendo na hali yoyote.
 4. kutanguliza anayoyapenda Allah kuliko yanayotakwa na nafsi mingoni mwa matamanio na matakwa.

{Atawapenda nao watampenda}

[Al maida:54]

 1. kutalii kwa moyo majina yake Allah yaliyomazuri na sifa zake na kuzijua.
 2. kushuhudia wema wake na ihsani yake na neema zake zilizo wazi nazilizofichika.
 3. Kudhalilisha moyo na kunyenyekea kabisa mbele yake Allah Mtukufu.
 4. kujitenga peke yako kwa ajili ya Allah usiku wa manane, wakati Allah anateremka katika mbingu ya dunia anajitenga kuwa pekee yakeili amuombe Allah, na asome kitabu chake Allah katika sala za suna, kisha anakamilisha sala yake hiyo kwa istighfaar kuomba msamaha na tawba.
 5. kukaa pamoja na wenye kumpenda [s.a.w]tena wakweli katika hilo, na kuvuna matunda mazurimazuri, maneno yao wakizungumza kama ambae wanachagua matunda mazuri, na kujizuia kuongea kama ila kama kutakuwa na maslahi na kujulikana kuwa kuna faida ya ziada kwake au kwa mwengine.
 6. kujiepusha na kila sababu inayoekambali moyo wake na Allah Mwenye nguvu na utukufu. 

Miongoni mwa matunda ya kumpenda Allah mja wake. 

 

Atakayempenda Allah, Allah humuongoza, na kumkaribisha . amesema Mtume[s.a.w]:«asema Allah Mtukufu “mimi niko kulingana na anavyo nidhania mja wangu, na niko naye atakaponikumbuka, basi akinikumbuka na kunitaja nafsini mwake, nitamkumbuka na kumtaja nafsini mwangu, na atakapo ni kumbuka na kunitaja mbele ya watu, ni tamtaja mbele ya walio bora [malaika] na akijikurubisha kwangu shibri moja nitamkaribia dhiraa moja na atakaponikaribia dhiraa moja nitamkaribia baa, na akinijia kwa kutembea nitamwendea kwa haraka haraka.» (Sahihi Albukhari)

Kila mja anavyo mcha Mola wake anazidi kupanda daraja katika uongofu zaidi, na kila ampendapo Allah humzidishia uongofu, na kila akiongoka zaidi huzidi uchaji Mungu wake.

Anaye mpenda Allah humuandikia kabuli [akakubaliwa] hapa ulimwenguni.

Inakusudiwa kabuli ya huyu mja hapa duniani: kumpendelea na kumridhia na kumtukuza, na kumfanya apendwe na kila kitu ila makafiri kwasababu walikataa kumpenda Allah, licha

kupenda vipenzi vyake. Amesema Mtume[s.a.w]«Allah atakapo mpenda mtu humuita Jibril [a.s] akamwambia: hakika ninampenda Fulani basi nawe mpende, akasema Mtume[s.a.w] basi Jibril naye humpenda huyo mja, kisha hunadi mbinguni akisema: hakika Allah anempenda Fulani basi nanyi mpendeni,viumbe vyote vya mbinguni navyo humpenda huyu mja kisha Allah anamuandikia huyu mja kabuli ardhini ya kukubaliwa na kupendwa na kila mtu»(Imepokewa na Muslim)

Hivi ndivyo inakuwa Allah akimpenda mja, humlinda na kumchunga na kujaalia kila kitu kumtii yeye na kumsahilishia kila gumu, na kumkaribishia kila lililo mbali, na humdhalilishia mambo ya kidunia akawa hahisi machovu yoyote ; asema Allah Mtukufu: {Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri[Mwenyezi Mungu] mwingi wa rehema atawafanyia mapenzi} [Maryam : 96]

Ampendaye Allah humfanya kuwa karibu naye, Allah akimpenda mja huwa naye akimlinda na kumchunga, na wala hamsaliti na yoyote hamuudhi wala hamdhuru, imekuja katika hadiith alqudsi” amesema Mtume[s.a.w] «Amesema Allah Mtukufu: mwenye kumfanyia uadui kipenzi changu nimemtangazia vita, na mja hajikaribishi kwangu nakitu ninacho kipenda ila kile nilicho wafaradhishia, Na hataacha mja wangu kujikurubisha kwangu kwa vitendo vya suna mpaka ni mpende, na nitakapompenda nitakuwa kama sikio lake lakusikizia au jicho lake lakuonea au mkono wake wakushikia au mguu wake wakutembelea, na atakapo niomba chochote nitampa na akiniomba kumuokoa nitamuokoa, na sija kuwa na kusitasita kwajambo ambalo lazima liwe ila katika kuchukuwa nafsi ya mja wangu, mja wangu anachukia kufa nami ninachukia kumuudhi mja wangu kwa kuchua roho yake» (Imepokewa na Albukhari)

Ampendaye Allah atakubaliwa maombi yake: miongoni mwa dalili za kupenda Allah waja wake waumini ni kukubali maombi yao, na kuwaneemesha kwa neema zake wanapoenua mikono yao tu

Imani ya kweli ni uhai wa roho na ni uwanja wa furaha, kama vile ukafiri ni mauti ya roho kabla ya kifo kikubwa, na uwanja wa huzuni.

kuielekeza mbinguni huku wakisema ewe Mola wetu, anasema Allah: {Na waja wangu watakapokuuliza hakika yangu,[waambie kuwa]mimi niko karibu nao. Naitika maombi ya mwombaji anaponiomba.basi na waniitikie na waniamini,ili wapate kuongoka.} [Albaqarah : 186]

Kutoka kwa Salmani Alfarsi alisema: alisema Mtume [s.a.w] «Hakika Allah ana haya sana tena mkarimu yuko na haya kutomkubalia mja wake anapoenua mikono akimuomba» (Imepokelewa na Tirmidhiyu).

Allah akimpenda mja ujalia malaika wakamtakia maghfira, malaika wanamuombea maghfira mtu anayependwa na Allah na wanamuombea kutoka kwa Allah rehema , anasema Allah : { Wale wanao beba A'rshi, na wanao izunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.}
[ALghaafir: 7]

Anasema Allah : {.Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [Shuura 5]

Allah anapompenda mja wake, anamfisha akiwa anaendelea kufanya vitendo na amali ..asema Mtume [s.a.w] «Allah akimtakia mja wake kheri anafungulia akaulizwa atamfungulia vipi akasema: anamfungulia na anamjalia na kumuafikia kutenda amali njema kabla ya mauti yake kisha anamtoa roho katika amali yake hiyo.»(Imepokewa na Ahmed)

Allah akimtakia mja wake kheri anampatia amani wakati wa kifo chake:

Allah akimpenda mja anampatia amani na utulivu duniani, na anamruzuku amani na thabati wakati wa kifo chake, anatumiwa malaika wakachuwe roho yake kwa upole na wanamthibitisha wakati wa kifo chake kwa kumbashiria pepo. Anasema Allah mtukufu: { Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.} [Fusilat :30]

Allah akimpenda mja wake anamjalia kuishi peponi milele. 

 

Ampendaye Allah atakuwa kesho akhera katika pepo, Allah amkirimu ampendaye huko akhera haijapita kwa akili ya mtu yoyote wa haitapita katika akili ya mtu yoyote,Allah

aliahidi waja wake anapowapenda kuwaingiza katika pepo yake , ndani yahiyo pepo mna kila chenye nafsi ina tamani kama ilivyokuja katika hadiith ya Mtume [s.a.w] «Nimewaandalia waja wangu wema mambo ambayo hamna jicho lililoona wala sikio lililosikia wala haijapita katika akili ya mtu ikoje hiyo pepo ya Allah.»{Nafsi yoyote haijui waliofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho [huko peponi]ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyafanya.} (Imepokewa na Albukhari)

Hakuna raha duniani ila kwa kumpenda Allah Mtukufu na kumtii yeye, wala haikamiliki raha ya peponi ila kumuona yeye .

Miongoni mwa matunda ya kumpenda Allah kwa mja ni kumuona Mola wake. 

 

Atadhihirika Allah kwa waja wake awapendao kwa nuru yake, na hawataona kitu wakipendacho zaidi ya kumuona Allah , kama ilivyo kuja kwa kauli yake Mtume [s.a.w] aliangalia mwezi usiku wa mwana mweupe akasema: «Hakika mtamuona Mola wenu kama mnavyo uona mwezi huu, hakutakuwa na kizuizi chochote katika kumuona, kama mtaweza kutoshindwa kuswali kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa basi mfanye hivyo, kisha akasema» [Sahihi bukhari] {Namtukuze mola wako kwa kumsifu, kabla ya kutoka jua,[sala ya asubuhi]na kabla ya kuchwa,[adhuhuri na alaasiri}
[qaf 39]

Hukmu na matanabahisho katika kupenda

 1. kumpenda Allah mja wake hakuzuii kumpatia mja wake mitihani, asema Mtume [s.a.w]«Hakika malipo makubwa yanalingana na ukubwa wa mitihani na Allah atakapo penda watu huwatia katika mitihani [misuko suko] basi mwenye kuridhia atapata radhi zake na mwenye kuchukia atakuwa na ghadhabu za Allah» (Imepokewa na Tirmidh)

Allah humtia mja wake katika misuko suko na mitihani mpaka amsafishe kutokana na dhambi zake na kuuacha moyo wake huru kutokana na shughuli za kidunia, amesema Allah Mtukufu: {Na tutakufanyieni mitihani mpaka tuwadhihirishe [wajulikane]wale wanaopigania dini miongoni mwenu na wanaosubiri; nasi tutadhihirisha habari zenu.} [Muhamad :31]

Akasema tena: {Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,* Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. * Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.} [Baqarah 155-157]

 1. Maasi ya mja kwa Mola wake yanapunguza mapenzi yake na kuyashusha chini na kuondoa ukamilifu wake, basi mapenzi ya Allah ni kama imani yako na msingi na yako na ukamilifu, sasa kulingana na maasi yanapungua mapenzi yake, na anapoingia mtu katika shaka na unafiki mkubwa yaondoka mapenzi yote ya Allah kwake, ambaye hamna moyoni mwake mapenzi ya Allah ni kafiri aliye toka katika uislamu au mnafiki mkubwa ambaye hana fungu lolote katika dini, ama wanao muasi Allah kwa madhambi ya kawaida hatuwezi kusema hawana mapenzi ya Allah , lakini twasema wako nayo lakini yamepunguwa, hivi ndivyo wanavyo amiliwa. Amesema Mtume [s.a.w]: «Kama nyinyi hamtendi dhambi basi Allah angeumba viumbe wengine wanaotenda dhambi kisha wanataka msamaha naye anawasamehe» (Imepokewa na Ahmad)

“Uhuru wa kikweli kweli ni uhuru wa moyo kutokana na korokoro za shirki na matamanio ya nafsi na shubha, na utumwa wa kikweli kweli ni utumwa wa moyo unapokuwa si wa Allah”

 1. mapenzi ya Allah hayazuii mapenzi ya kawaida ambayo nafsi hupenda kama kupenda chakula au kinywaji au kupenda wanawake au mengineyo. Asema Mtume [s.a.w] «Nimefanya duniani kupenda wanawake na manukato»
  (Imepokewa na Ahmed)

Kuna vitu duniani kuvipenda si shirki kwa sababu Mtume [s.a.w] mwenyewe alivipenda, kwahivyo yafaa mtu kupenda duniani vitu vyovyote bora tu visiwe ni haramu.

 1. mwenye kumpenda mtu yoyote kama vile anavyompenda Allah basi atakuwa ni mshirikina. Amesema Allah Mtukufu: {Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!} [Albaqarah 165]

Katika aya hii kuna makemeo makubwa kwa mwenye kuyafanya sawa mapenzi ya mtu na mapenzi ya Allah katika kuabudu na kutukuza.

Amesema Mtume [s.a.w]”hakika aamali bora inayopendwa na Allah ni kupenda kwa ajili ya Allah na kuchukia kwa ajili ya Allah” imepokewa na Ahmed

Amesema Allah Mtukufu {Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake.} [At tawba : 24]

Katika aya kuna kemeo kali kwa mwenye kuwa vitu hivi vinane ni vipenzi zaidi kwake kuliko Allah . kutoka kwa Anasi [r.a] amesema Mtume [ s.a.w] : «Hajaamini mmoja wenu paka anipende mimi zaidi ya anavyopenda wanawe au wazazi wake au watu wote»
(Imepokewa na Ibn Maajah)

 1. kuwapenda na kuwatukuza washirikina kuliko waislamu ni kinyume na mapenzi ya Allah, kwasababu ya ushirikina walionao washirikina na yeye kwasababu ya dini yake, kwahivyo kupenda ni kwa ajili ya Allah na kuchukia ni kwa ajili ya Allah, huu ndio msingi mkubwa katika misingi mikubwa ya imani. Asema Allah Mtukufu: {Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao}
  [Aali Imran : 28]

Allah akawakataza waumini kuwafanya makafiri kuwa wapenzi wao kisha aka kokoteza kuwa mwenye kufanya hivyo basi hatakuwa na chochote mbele ya Allah, kwasababu kumpenda Allah pamoja na kupenda maadui zake ni vitu ambavyo haviingiliani; {Ila kwa ajili ya kujinda na shari zao}[Aali Imran : 28]

Na Allah akaruhusu kuwafanyia urafiki kama mtu atakhofia shari zao akawa hawezi kuishi na amani ila afanye hivyo, hapo ndio itakuwa yafaa kuwafanya marafiki lakini urafiki wa dhahiri lakini moyoni mnachuki ya kuwachukia makafiri kwasababu ya iman yake.asema Allah Mtukufu: {Isipokuwa yule aliyeshurutishwa, hali ya kuwa moyo wake umetuwa juu ya uislamu wake} [An nahli: 106]

na uhakika wa mapenzi 

 

Alipokhiyarishwa Mtume [s.a.w] baina ya maisha ya dunia na baina ya kukutana na Allah Mtukufu. Akasema: « Nachagua kukutana na Allah aliye juu» (Imepokewa na Ahmad)

Akachagua mapenzi ya Allah Mtukufu na mapenzi ya kukutana naye, akayatanguliza kuliko mapenzi ya dunia na matamanio yake na ladha zake.

Alama za kumpenda Allah ni kumtaja sana na kuwa na shauku ya kukutana naye, kwasababu mtu akipenda kitu hukithirisha kukitaja na hupenda kukutana nacho.

Kutoka kwa Rabii’I Ibn Anas 

 

Marejeo

 1. eleza ni nini mapenzi?
 2. taja athari za mapenzi yako kwa Allah Mtukufu kwako na maishani mwako.
 3. je yawezekana kuabudiwa Allah kwa mapenzi pekee bila kuogopewa na kutarajiwa thawabu zake? Lete dalili kwa maneno uyasemayo katika maisha ya manabii.
 4. Hupata nini mja atakapopendwa na Allah?
 5. eleza uhusiano ulioko baina ya majina ya Allah na sifa zake uzijuazo na mapenzi yake?