Maana ya (arrabu) Mola Mlezi

Maana ya (arrabu) Mola Mlezi

MaaNa ya (arrabu) Mola Mlezi

Allah ….Ni Jina Lililo Tamu Kulitamka Maanayake Shuari, Yapaswa Kulipenda Kushikamana Nalo Kwa Kumpwekeshea Mwenyewe Allah Ibada Na Kuachana Kuabudu Chochote ILA Yeye Pekee, Ni Ubora Ulioje Huu!

{Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Muumbaji, Mfanyaji WA Sura Tofauti Tofauti} (Al-Hashr: 24)

Al-Rrabu: Ni Bwana Asiye Na Mfano, Mwenye Kutengeza Mambo Ya Waja Wake Kwa Neema Alizo Wapa, Mfalme Anayeumba Na Kuamrisha. Jina Hili La Arrabu Haliitiwi Mwanadamu Ispokuwa Kwa Kuegemeza, Mfano (Rrabu-Ddari) Mwenye Nyumba, (Rrabul-Maali) Mwenye Mali, Yaani Mwenye Kuimiliki, Ama Likija Bila Kiegemezo Chochote Basi Nilake Allah Pekee.

Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Muumbaji Mwenye Kutoa Sura Tofauti Tofauti, Aliyeumba Kila Kinacho Patikana Na Ndiye Wa Mwanzo Kuumba Vitu Hivi Bila Ya Mfano Kisha Kaviweka Sawa Kwa Hikima Yake, Akavivisha Sura Nzuri Kwa Neema Zake, Naye Bado Anasifika Na Sifa Hii Kubwa.

Ilipokuwa Elimu Ya Watu Kwa Haja Zao Na Kumuhitaji Kwao Arrabu (Mola Mlezi) Ni Zaidi Kabla Kumuhitaji Allah Mwenye Kuabudiwa , Na Kumkusudia Kwa Haja Zao Za Karibu Na Za Mbali, Ilikuwa Kuukubali Uungu Wa Allah Kabla Kukubali Kumfanyia Yeye Ibada, Wala Kabla Ya Kumuomba Na Kutaka Kuokolewa Na Kumtegemea, Ni Zaidi Kuliko Kumuabudu Na Kumtaka Msamaha.

Allah Mlezi: Ndiye Mwenye Kulea Viumbe Vyake Vyote Kwa Mpangilio Maalum, Na Aina Tofauti Tofauti. Na Malezi Maalumu Kwa Waja Wake Aliowachagua, Kwa Kuzifanya Nyoyo Zao Safi Na Kutengeza Tabia Zao, Ndio Maana Zikawa Dua Zao Zinaanza Na Jina Hili La Al-Rrabu, Kwa Sababu Wanataka Kutoka Kwake Malezi Haya Maalumu.

Na Jina Al-Rrabu Linabeba Maana Mazito Sana, Yakiwemo Kupanga Mambo Ya Viumbe, Kuruzuku, Kutoa Afya, Na Kumuwafikia Mtu, Na Kumthibitisha Katika Usawa. Amesema Allah Mtukufu: {Na Ambaye Ndiye Anayenilisha Na Kuninywesha. Na Ninapougua, Yeye Ndiye Ananiponesha. Na Ambaye Atanifisha Kisha Atanihuisha} (Ash-Shuaraa: 79-81)



Tags: