Allah Mpole

Allah  Mpole

Allah Mpole

Hakika Allah Ni Mpole: {Hakika Mola Wangu Mlezi Ni Mpole Kwa alitakalo.} (Yusuf: 100)

&"Mpole&" …Ambaye ameWafanya viumbe kuWa Wapole Kwa wenzao Na upendo Na kusikitiaNa.

&"Mpole&"… Mwenye kutoa wema mwingi Na zaWadi kubWa kubWa.

&"Mpole&" …Mpole Kwa Waja Wake {Mwenyezi Mungu Ni Mpole Kwa Waja Wake} (Ash-shuraa: 19)

ANaWapa yaliyokuWa ya kheri kWao katika duNia Yao au akhera Yao, Na aNaWanyima Na kuWazuia yaliyo mabaya kWao katika diNi Yao Na duNia Yao.

&"Mpole&"… Macho hayamfikilii Bali Yeye aNayafikilia macho. {Macho hayamfikilii Bali Yeye aNayafikilia macho. Naye Ni Mjuzi, Mwenye khabari. } (Al-an’am: 103)

“Mpole” ANajua yaliyo fichika, Na aNahesabu vitendo vidogo, hakifichiki kWake chochote usiku Wala mchaNa, aNayajua maslahi ya Waja Wake madogo Kwa makubWa Na aNaWafanyia upole.

“Mpole”…Ambaye elimu yake imeenea vitu vyote, vya siri Na vilivyojificha, Na akajua yaliyo fichika ndaNi ya vitu vidogo, Mpole Kwa Waja Wake Waislamu. ANaye Wafikishia maslahi ya upole Wake Na wema Wake Kwa njia Wasizotarajia.

“Mpole”… Ni Mpole Kwa Waja Wake aNapohukumu katika jambo FulaNi, Na aNaWasaidia akikadiria jambo, Na aNaWafungulia milango ya faraja mambo yakijifunga Na yakiWa magumu, Na aNaWafanyia wepesi mambo yakiWa magumu ametakasika Allah.

Hakika yeye Ni Allah Mpole…Tags: