Ikhlasi huwa vipi?

Ikhlasi huwa vipi?

Ikhlasi huWa vipi?

Moja: kuhakikisha kumpwekesha Allah Mtukufu, amesema Allah Mtukufu: {ukimsafia DiNi Yeye Tu. . .* Hakika DiNi Safi Ni ya Mwenyezi Mungu Tu.} (Az-zumar: 2-3)

Kila kilicho ndaNi kiNachoenda kinyume Na cha nnje, Ni batil.

Amesema Allah Mtukufu: {Nao haWakuamrishWa kitu ILA Wamuabudu Mwenyezi Mungu Kwa kumtakasia DiNi,} (Al-bayiNa: 5)

Pili: kuhakikisha kumfuata Mtume WA Allah (s.a.w) kumtii katika alyoamrisha, Na kujiepusha Na aliyo yakataza Na kuyakemea. ANasema Allah Mtukufu: {Enyi mlio amiNi! Mt&" iiNi Mwenyezi Mungu, Na mt&" iiNi Mtume Na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozaNa katika jambo basi lirudisheNi Kwa Mwenyezi Mungu Na Mtume, ikiWa mNamuamiNi Mwenyezi Mungu Na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi Na ndiyo yenye mwisho mwema. } (An-Nisaa: 59)

Tatu: kama uNataka kuWa Mwenye ikhlasi jaribu kuchunga a’amali zako nzuri, Na ukumbuke daima Watu saba ambao WatakuWa chiNi ya kivuli cha Allah siku ambayo hakutakuWa Na kivuli isipokuWa chake Allah: “Na mtu ambaye aNatoa sadaka kWa mkono Wake Wa kulia Na akaificha paka mkono Wake Wakushoto usijue kilichotoleWa Na mkono Wa kulia” (ImepokeWa Na Albukhari), Na ukumbuke pia: “Hakika kila kitu kiNazngatiWa Nia “ (ImepokeWa Na Albukhari)

NNE: Wacha kupenda sifa Na kushukuriWa Na umashuhuri, Na kata tamaa kabisa Na vitu vilivyomo mikonoNi mWa Watu, Na tengeneza usiano Wako Na Mola Wako. KWasababu mwenye ikhlasi hawi Na tamaa Na pato la kiduNia au mke Wakuoa, lakiNi tamaa yake iko Kwa rehema za Allah.

Tano: Ni juu yako kujiangusha mbele ya Mola Wako, Na kujilazimisha Na udhalilifu mbele ya mlango Wake Allah Mwenye nguvu Na utukufu Kwa kumuomba akuruzuku Na akupe ikhlas, Na akuepushe Na kujinesha, Na akutubie kWa yaliotangulia mwenye madhambi Na maasi.

Ikhlasi Ni kutotaka katika a’amali yako shahidi isipokuWa Allah, Na Wala kutotaka Mlipajimwengine asiyekuWa yeye.

Sita: kujiepusha Na RIA (kujionesha) Na kuWa Na tahadhari kWayo, mja atakapojua njia ya riaa Na maingilio yake, mtu uweza kujiepusha Na vivunja ikhlasi, miongoNi mWazo kujisifu Kwa baadhi ya Watu kWamba Wao Ni maWalii, ama kuridhia kuitWa maWalii, ama kusimulia matendo yake Na tWaa yake,

Asema Allah Mtukufu: {WaNao taka maisha ya duNia Na pumbao lake tutaWalipa humo vitendo vyao kaamili. Na Wao humo haWatopunjWa. ***Hao ndio ambao haWatakuWa Na kitu Akhera ILA Moto, Na yataharibika Waliyo yafanya, Na yatapotea bure Waliyo kuWa Wakiyatenda.} (HUD: 15-16)

Kujionesha Ni shirki ndogo Na iNatosha kuWa Na mwisho m‘baya WA kutokubaliWa vitendo hata Kama Ni vyema dhahiri yake Na kurudisha Kwa wenyewe, Saba: kusuhubiaNa Na Watu wema: amesema Mtuse (s.a.w) “Mtu yuko katika diNi ya sahibu Wake” (ImepokeWa Na Tirmidh)

Nane: kuificha ibada Na kuifanya siri. Asema Allah Mtukufu: {Mkizidhihirisha sadaka Ni vizuri; Na mkizificha mkaWapa mafakiri Kwa siri basi hivyo Ni kheri kwenu,} (Al-baqarah: 271)

Tisa: kujiesabu Nafsi yako Kwa hali ya juu Sana, Nako Ni kujihesabu ambako kuNalazimiaNa Naye katika kila a’amali Wakati wowote, amesema: Allah Mtukufu: {Na WaNao fanya juhudi Kwa ajili yetu, Sisi tutaWaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja Na Watu wema.} (Al-ankabut: 69), Ebu zingatia neon lake Allah: {Kwetu!!}

HavikutaNi moyoNi viwili: kupenda sifa Na kutajWa pamoja Na ikhlasi, Kama vile ambavyo maji Na moto hayawezi kukuteNa.

kumi: kumuomba Allah Na kumuelekea yeye Na kuendelea hivyo, kWasababu mja Ni fakiri atakapo uelekea mlango Wa BWaNa Wake humuonea huruma Na kumrehemu Na humkidhia haja yake Na aNachokiomba Na kumuondoshea mahitaji yake, kWahio dua Ni kumuomba Allah Mwenye nguvu Na Utukufu.



Tags: