MATUNDA YA Ikhlas

MATUNDA YA IMANI

MATUNDA YA IMANI

Anasema Allwah Mtukufu {Huoni Mwenyeezzi Mungu Alivopiga Mfano Wa Neno Zuri Ni Kama Mti Ulio Mzuri Asli Imejik’ita Ardhini Na Utanzu Wake Uku Mbinguni, Hutowa Vyakula Vyake Kila Mara Kwa Idhni Ya Mola Wake.} (Ibrahim: 24-25)

Na Miongoni Mwa Matunda Ya Imani Ni Kama Yafuatavyo:

1-Imani Ya Kweli Hutia Utulivu Na Raha Ya Nafsi Na Ukunjufu WA Kifua. Na Hili Linasadikisha Neno Lake Mwenyeezzi Mungu {Juwa Kwamba WA Penzi WA Mwenyeezzi Mungu Hawana Kicho Wala Hawatahuzinika} (Yunus 62)

2-Ni Kupata Waumini Upamoja Makhsusi Kutoka Wa Mwenyeezzi Mungu , Yaani Huwatoa Kwenye Giza Ka Ukafiri Na Shida Zake Kuwapeleka Kwenye Nuru Ya Imani Na Thawabu Zake

3-Kufaulu Kwa Kupata Radhi Za Allah Na Pepo Yake Aliyo Waandalilia Waumini Wake Wakikweli Kweli. Kasema Allah Mtukufu: { Mwenyezi Mungu Amewaahidi Wanaomuamini Wanaume Na Wanawake (Amewaahidi) Mabustani (Pepo) Zipitazo Mito Mbele Yake Kukaa Humo Daima, Na Makazi Mazuri Katika Mabustani Hayo Yenye Kudumu, Na Radhi Za Mwenyezi Mungu Ni Kubwa Zaidi. } (At-Tawba: 72)

4-Allwah Anawahifadhi Na Kuwakinga Vipenzi Vyake: {Hakika Mwenyezi Mungu Huwatetea Walio Muaamini} (Al-Hajj: 38)

Miongoni Mwahayo: Allwah Kumkinga Mtume Wake Muhammad (S.A.W) Katika Tukio La Kuhama Kwake Na Jinsi Allwah Alimuhifadhi Ibrahim (A.W) Alipotupwa Ndani Ya Moto.

Kumuamini Allwah Ni Uhusiano Baina Ya Mja Dhaifu Na Mola Wake, Kama Vile Mwenye Nguvu Naye Pia Umuomba Allwah.

5-Utukufu Katika Dini Na Uongozi Kwenye Hiyo Dini, Amesema Mwenyeezzi Mungu (S.W): {Na Tukawafanya Miongoni Mwao Maimamu Wanaoongoza Kwa Amri Yetu Walipo Subiri} (As-Sajda 24)

Hakuna Dalili Kubwa Ya Hilo Kuliko, Utawala WA Watu WA Dini Na Yaqini Juu Ya Allwah, Allwah Ameendleza Matukufu Yao Na Wao Wako Chini Ya Matabaka Ya Michanga, Miili Yao Imekosekana Lakini Athari Zao Na Habari Zao Ziko Kwenye Maisha.

6-Mapenzi Ya Allwah Kwa Waumini, Amesema Allwah: {Mwenyezi Mungu Anawapenda Nao Wanampenda} (Al-Maaida: 54)

Na Amesema Allwah Mtukufu: {Hakika Wale Walioamini Na Kufanya A’amali Mzuri (Mwenyezi Mungu) Atawapa Upendo} (Maryam: 96)

Uhayi Pasina Imani Ni Mauti Yasiyo Shaka... Mboni Pasina Imani Ni Up’ofu. Ulimi Bila Imani Ni Ububu. Mkono Bila Imani Ni Mlemavu.

7-Maisha Mazuri Ya Dunia Na Akhera, Allwah Mtukufu Amesema: {Yoyote Mwenye Kufanya Mema, Awe Mume Au Mke, Na Hali Yeye Ni Mwenye Imani Tutampa Maisha Mazuri Na Tutawajazi Malipo Yao Kwa Vyema Kuliko Walivo Fanya.} (An Nahl 97)

Basi Wako Wapi Wenye Kutafuta Maisha Mazuri Na Furaha?

8-Mapenzi Ya Allwah Kwa Muumin Na Mapenzi Ya Muumin Kwa Allwah, Anasema Allwah: {Mwenyezi Mungu Anawapenda Nao Wanampenda} (Al Maaida 54)

Yaani Anawapenda Na Anawawekea Mahaba Kwa Watu.

9-Kupata Bishara Nzuri Kwa Watu WA Imani Kwa Ukarimu WA Allwah Kwao .Allah Mtukufu Asema: {Wabashirie Waumini} (At Tawbah: 112)

Wala Hakutolewi Bishara Illa Kwa Jambo Kubwa, Athari Yake Ikadhihiri Juu Ya Ngozi Ndipo Ikaitwa Bishara Wala Hakuna Kikubwa Kuliko Rehma Ya Mwenyeezzi Mungu Na Radhi Zake Na Pepo Yake, Anasema Allwah: {Wabashirie Walioamini Na Wakafanya Mema Kwamba Wana Mabustani Yanayo Pita Chini} (Al Baqarah 25).

10-Imani Ni Sababu Ya Kuthubutu, Anasema Allah Mtukufu: { Wale Ambao Watu (Waliwatisha) Wakawaambia, Watu Wamewakusanyia, Waogopeni (Hilo) Likawazidishia Imani Na Wakasema Tosho Letu Ni Mwenyeezzi Mungu Alie Mwema Wakutegemewa } (Aal Imran 173)

Wala Hakuna Ambalo Ni Dalili Kubwa Ya Kuthubutu Huku Kuliko Yale Yaliyo Andikwa Na Tarikhi Kuhusu Mitume Na Maswahaba Na Waliofuatia Wao, Na Alie Kwenda Juu Ya Mwendo Wao.

11-Kufaidika Na Mawaidha, Anasema Allwah Mtukufu: {Basi Wakumbushe, Kukumbusha Kunawafaa Waumini} (Adhariyat: 55), Hawafaidiki Na Mawaidha ILA Watu WA Imani.

12-Amiweka Kheri Kwa Hali Zote Kwa Mwenye Imani, Katika Hali Ya Furaha Na Katika Hali Ya Dhiki, Kheri Huwa Ni Yenye Kuambatana Na Muumin: &"Ni Ajabu Mambo Ya Muumin Hali Zake Zote Kwake Ni Kheri Halipatikani Hili Ila Kwa Muumini, Akipata Mazuri Hushukuru Ikawa Kheri Kwake, Na Yakimsibu Madhara Husubiri Ikawa Kheri Kwake.&" (Imepokewa Na Muslim)

Kwahiyo Imani Inampeleka Mtu Kuwa Na Subra Wakati WA Madhara, Na Kushukuru Wakati WA

13-Kuhifadhiwa Muumin Na Kuingia Katika Madhambi Makubwa, Limeswihi Neno Lake: Mtume (S.A.W) “Hazini Mwenye Kuzini Ila Huwa Hana Imani Wakati Huo” (Imepokewa Na Bukhari)

Haya Ni Matunda Mema Ya Ubora WA Imani, Basi Wako Wapi Wenye Kutafuta Kusuudika Na Raha Ya Moyo Na Utulivu

ATHARI ZA IMANI:

Miongoni Mwa Athari Za Imani Kwa Maisha Ya Muumin:

1-Kuongezeka Pupa Ya Muumin Katika Kufuata Sharia Tukufu, Asema Allah Mtukufu { Haiwi Kauli Ya Waislamu Wanapoitwa Kwa Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Ili Ahukumu Baina Yao, ILA Husema:”Tumesikia Na Tumekubali,”Na Hao Ndio Wenye Kufaulu} (An-Nur 51)

Basi Imani Humpeleka Mwenye Nayo Kwenye Kufanya Haraka Kufuata Na Kunyokea Amri Ya Mwenyeezzi Mungu , Asema Allah Mtukufu { Basi Sio Naapa Kwa Mola Wako Hawatoamini Mpaka Wakufanye Wewe Ndie Hakimu Wao Kwenye Utesi Uliozuka Kati Yao Kisha Wasipate Katika Nyoyo Zao Shida Kwa Ulilohukumu Na Wajisalimishe Kabisaa. } (An-Nisaa: 65)

Bali Imani Inampelekea Muumin Kusalimu Amri Na Kuridhia Na Amri Za Allwah Mtukufu.

Kumuamini Allwah Ni Uhayi ... Na Uhayi Pamoja Na Mungu Ni Kuamini.

2-Humuhifadhi Mwenyeezzi Mungu Mja Wake Na Shirki Wazi Na Ilojificha , Na Nikatika Hayo: Kutopeleka Cha Maombi Chochote Au Chakutaka Msaada Au Kutaka Kuokolewa Popote Kwa Asie Kuwa Mwenyeezzi Mungu, Mwenye Kunufaisha Na Mwenye Kudhuru Ni Allwah: { Na Akikugusa Mwenyeezzi Mungu Kwa Madhara Yoyote Hakuna Mwenye Kuyaondoa Asie Kuwa Yeye } (Al An-Am 17)

3-Kupenda Na Kuchukia Kuwe Kwa Ajili Ya Allwah, Na Hiyo Ndiyo Kamba Imara Mno Ya Imani, Anasema Allwah Mtukufu: {Hakika Waumini Ni Ndugu} (A-Lhujuraat: 10)

Wala Hakuna Dalili Kubwa Kwa Hilo Kuliko Kuwafanya Ansari Na Muhajirina Ni Ndugu, Na Kujitolea Kwao Nafsi Zao Na Malo Yao Kuwapa Ndugu Zao, Alisema Mtume (S.A.W) “Hatuamini Mmoja Wenu Mpaka Ampendele Nduguye Analo Jipendelea.” (Amepokea Bukhari)

{Enyi Mlioamini Aminini}Aliwaita Kwenye Imani Na Kuwahimiza Kwasababu Ya Ubora Wake.

4-Kusubiri Kwenye Jihadi Kwa Ajili Ya Mwenyeezzi Mungu Na Kutoa Vilio Ghali Na Vitukufu Kwa Ajili Ya Kumridhisha Allwah, Anasema Mtukufu : { Hakika Waumini Tu Ni Wale Walio Muamini Na Mtume Wake Kisha Wasifanye Shaka Na Wakapigana Jihadi Kwa Mali Yao Na Nafsi Zao Katika Njia Ya Allwah Hao Ndio Wa Kweli. } (Al-Hujurat 15)

5-Moyo Kuambatana Na Mungu Na Ahadi Yake Na Kusuudika Kwake Kwa Hilo, Pepo Ya Ulimwengu Kwake Yeye Ni Kuamni Na Kumtii Allwah, Na Ataraji Pepo Ya Aakhera Ambayo Ni Ahadi Ya Mwenyeezzi Mungu Kwake, Kamwe Ataraji Thawabu Ya Mwenyeezzi Mungu Kwa Kila Limkumbalo Katika Shida Na Tabu Na Usumbufu, Na Yaandikwe Kwenye Aamali Zake, Anasema Allwah: {Haikuwa Sawa Kwa Watu Wa Madina Na Walio Pambizoni Mwao Miongoni Mwa Mebedui Wabaki Nyuma Wasende Na Mtume, Wala Wajipendele Wao Kuliko Kumpendelea Yeye Hilo Ni Kwakuwa Haiwasibu Wao Kiu Wala Sumbuko Wala Shida Katika Njia Ya Mwenyeezzi Mungu, Wala Hawakanyagi Popote Penye Kuwatia Hasira Makafiri Wala Hawamtii Adui Utungu Wowote Isipokowa Huandikiwa Wao Kwa Hilo Aamali Njema Wala Mwenyeezzi Mungu Hapotezi Malipo Ya Wenye Kutenda Wema. Wala Hawatoi Chochote Kidogo Wala Kingi Wala Hawakati Wangwa (Kwa Safari) ILA Huandikiwa Wao Ili Awalipe Wao Mema Mno, Yayale Wailokuwa Wakiyafanya.} (At Tawba 120-121)

Yote Haya Ni Ya Watu WA Walio Muamini Allwah Na Wakamswadikisha Katika Matendo Yao.

6-Kupata Uwalii (URAFIKI) Wa Allwah Na Mtume (S.A.W) Aesema Allah Mtukufu: {Rafiki Yenu Khasa ( Wakumsafia Nia ) Ni Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Na Waliomini Ambao Husimamisha Sala Na Hutoa Zaka, Na Hali Yakuwa Wananyenyekea.} (Al Maidah 55)

Uwalii Wa Allwah Ni ; Kumpenda Allwah Mtukufu Na Kunusuru Dini Yake Na Kuwapenda Mawalii Wake Na Kuwakata Wote Wasiokuwa Hawa Kwasababu Ni Maadui Wa Allwah Mtukufu .

Amesema Allah Mtukufu : {Huwapati (Huwaoni) Watu Wanaomuamini Mwenyezzi Mungu Na Siku Ya Mwisho, Kuwa Wanawapenda Wale Wanaompinga Mwenyezzi Mungu Na Mtume Wake; Hata Wakiwa Ni Baba Zao Au Watoto Wao Au Ndugu Zao Au Jamaa Zao. Hao Ndio Ambao (Mwenyezzi Mungu) Ameandika (Amethibitisha Kweli Kweli) Nyoyoni Mwao Imani Na Atawaingiza Katika Mabustani Yapitayo Mito Mbele Yake; Humo Watakaa Daima. Mwenyezi Mungu Amekuwa Radhi Nao, Na Wao Wamekuwa Radhi Naye. Hao Ndio Kundi La Mwenyezzi Mungu Ndilo Linalofaulu.} (Al-Mujadilaa 22)

Muumini Anampenda Allwah Na Mtume Wake Na Waumini Wote Na Wala Hawafanyi Makafiri Kuwa Marafiki Wake Katu, Asema Allwah Mtukufu: { Walioamini Wasiwafanye Makafiri Kuwa Wapenzi Wao ( Wa Kuwapa Siri Zao) Badala Ya (Waislamu Wenziwao). } (Aali Imran 28)

7-Kupata Tabia Nzuri, Imethibiti Kutoka Kwa Mtume (S.A.W) &"Haya Na Imani Yaenda Pamoja, Ikiondoka Moja Yapili Nayo Yaondoka.&" (Imepokewa Na Baihaqi)

Na Sifa Ya Haya Ni Miongoni Mwa Tabia Nzuri Muumini Anajaribu Kutengeza Muamala Wake Na Ndugu Zake Waislamu Ili Aishi Katika Neema Za Dunia Bila Mashaka Wala Chuki… Yote Haya Kwasababu Yeye Ni Muumin, Hayapatikani Haya ILA Kwa Muumin.

8-Furaha Ya Hakika Na Raha Halisi Ya Moyo, Kiwango Ambacho Anahisi Kuwa Yuko Peponi Haliyakuwa Yuko Duniani Kwa Sababu Ya Raha Anayo Ihisi Katika Utulivu Wa Moyo, Kwa Sababu Yuko Na Allwah Mmoja Pekee Na Mtume Mmoja Ni Muhamad (S.A.W) Na Njia Moja Nayo Ni Kufuata Radhi Za Allwah Na Lengo Moja Ni Pepo Iliyo Na Mapana Kama Mbingu Na Ardhi.

Hakika Siku Hizi Unaona Zahanati Nyingi Za Ungonjwa Wa Nafsi Kila Mahali, Zilizo Jaa Wagonjwa Wa Nafsi Kila Mtu Analia Kutopata Utulivu Wa Moyo Na Wasiwasi Na Mstuko Wa Roho Na Kukosa Usingizi, Hapo Ndipo Ujuapo Kwa Yakini Yote Haya Nisababu Ya Kuwambali Kwao Na Imani Ya Allwah Ya Uhakika Wake, Na Sababu Ya Kuegemea Dunia Na Kufungamana Nayo Sana, Kwasababu Kupenda Vitu Kumeingia Ndani Ya Nyoyo Zao. Mwanadamu Anahitaji Sana Kupata Chakula Cha Moyo Na Haya Hayawi Ila Kwakuamini Imani Ya Haki Na Kushikana Nayo Na Kudumu Kuitaja Na Kuamini Malaika Na Vitabu Vitakatifu Na Mitume Na Kuamini Siku Ya Mwisho Na Qadari Nzuri Au Shida Zote Zatoka Kwa Allwah.

Lakuzingatia Ni Kuwa Watu Wengi Wameghafilika Na Dawa Ya Moyo Na Utulivu WA Moyo, Na Pepo Ya Dunia Na Wakaelekea Nyuma Ya Mapato Ya Dunia Isio Dumu Ndio Maana Haija Wakamilishia Waliyo Yataka Wala Hawajawahi Kupumzika Tokea Mwanzoni Mwa Njia.

Na Kutosheleza Matakwa Ya Moyo Hayapatikani Ila Kwa Imani, Kwa Sababu Moyo Umetoka Kwa Allwah, Na Mwili Aliwuumba Allwah Kutokana Na Mchanga, Kila Zitakapotosheka Nyoyo Kwa Imani Hupatikana Heshima Na Utukufu Na Hutulia Na Hujiepusha Na Mambo Yasiokuwa Na Faida, Na Kila Likisahulika Hili La Kuitosheleza Nafsi Kwa Imani, Anakuwa Mwanadamu Kama Mnyama Mwenye Kushindwa Na Matamanio Ya Nafsi Yake Na Kupata Dhiki Na Unyonge.



Tags: