KUAMINI MITUME WA ALLWAH WALIO MTANGAZA .

KUAMINI MITUME WA ALLWAH WALIO MTANGAZA .

KUAMINI MITUME WA ALLWAH WALIO MTANGAZA

Hakuumba Allwah Waja Wake Bure Tu Bila Sababu, Na Wala Hakuwaacha Bure, Ndipo Aliwatumia Mitume Wake Ili Wamtangaze Allwah, Na Utukufu Wake, Na Ukamilifu Wake, Na Kutangaza Sharia Zake, Na Allwah Ametuma Katika Kila Watu Mbora Wao ,Akatuma Mitume Mingi Sana Miongoni Mwao: Nuh Ibrahim,Musa,Issa, (A.S) Na Mwisho Akamtuma Mwisho Wa Manabii, Mbora Wa Viumbe Wote Muhamad (S.A.W) Na Akawapatia Kila Mmoja Miujiza Yake Yenye Kujulisha Ukweli Wao, Wakafikisha Amana, Na Wakatekeleza Jukumu La Utume, Na Wakawafahamisha Waja Kuhusu Mola Wao Na Muumba Wao, Basi Asie Amini Risala Yao Na Kutokubali Hajamuamini Allwah. Amesema Allah: {Mtume Ameamini Yaliyoteremshwa Kwake Kutoka Kwa Mola Wake, Na Waislamu, (Pia Wameamini Hayo): Wote Wamemwamini Mwenyezi Mungu, Na Malaika Wake Na Vitabu Vyake, Na Mitume Yake} (Al Baqarah 285)

Kwasababu Wao Ndio Walio Tufikishia Ujumbe WA Allwah Mtukufu Kwahiyo Tunawaamini Wote. Allah Amesema: {Hatutafautishi Baina Ya Yoyote Katika Mitume Yake (Wote Tunawaamini)} (Al Baqarah 285)

Allwah Mtukufu Ametuma Hawa Mitume Pamoja Na Vitabu Ili Viwe Nuru Kwa Wanadamu, Akatuma Pamoja Na Nabii Ibrahim Sahifa Na Pamoja Na Nabii Daudi Zabuur Na Pamoja Na Nabii Na Musa Taurat, Na Pamoja Na Nabii Issa Injil Na Pamoja Na Mtume Muhamad (S.A.W) Quran Kitabu Kilicho Na Miujiza: {Hiki Ni Kitabu Ambacho Aya Zake Zimetengenezwa Vizuri, Kisha Zikapambanuliwa (Vyema) Kutoka Kwa (Mwenyezi Mungu) Mwenye Hikima Na Mwenye Ujuzi Wa Kila Kitu.} (HUD 1)

Amekifanya Allah Kuwa Ni Uongofu Na Nuru Na Baraka Na Dalili. Asema Allah Mtukufu: {Na Hii Qurani Ni Kitabu Tulichokiteremsha (Kwenu), Kilicho Na Baraka Nyingi. Basi Kifuateni Na Muwe Wacha Mungu Ili Mrehemewe} (Alan-Am 155)

Na Akasema Tena: {Enyi Watu! Imekufikieni Dalili Kutoka Kwaa Mola Wenu, Na Tumekuteremshieni Nuru Iliyo Dhahiri} (An Nisaa 174)

Allwah Amejalia Kuamini Mtume Muhamad (S.A.W.) Na Kuamini Ujumbe Wake Kuwa Pamoja Na Kumuamini Yeye Pekee, Katika Kalma Ya Shahada Ambayo Ni Kushuhudia Kuwa Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Illa Allah, Na Kushuhudia Kuwa Muhamad (S.A.W) Ni Mtume Wake, Amemtuma Allwah Mtukufu Kuwa Rehema Ya Walimwengu, Akawatoa Kutoka Giza Paka Kwenye Nuru, Na Kutoka Kwa Ujahili Paka Kwa Elimu Na Kutoka Kwa Upotevu Paka Kwenye Uongofu, Akafikisha Amana Na Akawanasihi Watu Na Alikuwa Na Pupa Juu Ya Umma Wake , Amesema Allah Mtukufu: { Amekufikieni Mtume Aliye Jinsi Moja Na Nyinyi, Yanamuhuzunisha Yanayokutaabisheni, Anakuhangaikieni. (Na) Kwa Walioamini Ni Mpole Na Mwenye Huruma} (At Tawba 128)

Allah Akampa Mtume Wake Miongoni Mwa Haki Anazostahiki, Yeye Ni Mbora Wa Viumbe Vyote Na Bwana Wao, Asema Mtume (S.A.W) &" Mimi Ni Bwana Wa Watoto Wa Adam Wala Sikujisifu.&" (Imepokewa Na Ibn Maja)

Na miongoNi mWa haki zake:

1-Kuamini Yeye Ni Mja Wa Allah Na Mtume Wake Na Allah Amemtuma Kuwa Rehema Kwa Waja Wake, Na Alifikisha Amana, Na Akatekeleza Risala , Asema Allah Mtukufu: {Basi Muaminini Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Na Nuru Tuliyoiteremsha,(Qur’an)} (Taghaabun 8)

Amesema Mtume (S.A.W) “ Naapa Na Yule Ambaye Nafsi Ya Muhamad Iko Mikononi Mwake Hakuna Atakaye Sikia Ujumbe Wangu Huu Miongoni Mwa Watu Wa Uma Huu Awe Yahudi Au Mkristo Kisha Afe Bila Kuamini Niliyo Kuja Nayo Ispokuwa Atakuwa Ni Mtu Wa Motoni “ (Imepokewa Na Muslim)

2-Kukubali Na Kusadikisha Aliyokuja Nayo Kutoka Kwa Mola Wake Mtukufu Na Kuyakinisha Kwamba Ni Haki Kutoka Kwa Allah Mtukufu Bila Shaka. Asema Allah Mtukufu: { Wenye Kuamini Kweli Kweli Ni Wale Waliomuamini Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Kisha Wakawa Si Wenye Shaka } (Al-Hujurat 15)

Amesema Allah Mtukufu: { Naapa Kwa Mola Wako, Wao Hawawi Wenye Kuamini (Kweli Kweli) Mpaka Wakufanye (Wewe Ndiye) Hakimu (Mwamuzi )Katika Yale Wanayokhitalifiana, Kisha Wasione Uzito Nyoni Mwao Juu Ya Hukumu Uliyotoa, Na Wanyenyekee Kabisa } (An Nisaa 65)

3-Kumpenda Mtume (S.A.W) Asema Allah Mtukufu { Sema:”Kama Baba Zenu Na Wana Wenu Na Ndugu Zenu Na Wake Zenu Na Jamaa Zenu Na Mali Mlizochuma Na Biashara Mnazoogopa Kuharibikiwa, Na Majumba Mnayoyapenda;(Ikiwa Vitu Hivi) Ni Vipenzi Zaidi Kwenu Kuliko Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Na Kupigania Dini Yake, Basi Ngojeni Mpaka Mwenyezi Mungu Alete Amri Yake; Na Mwenyezi Mungu Hawaongozi Watu Maasi} (At Tawbah 24)

Na Akasema Mtume (S.A.W) “Haja Amini Mmoja Wenu Paka Niwe Kipenzi Chake Zaidi Ya Wazazi Wake Na Watoto Wake Na Watu Wote” (Imepokewa Na Bukhar)

4-Kumuheshimu Na Kumtukuza Allah , Amesema Allah: { Ili Mumuamini Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake, Na Mumsaidie, Na Mumhishimu, Na Mumtakase Asubuhi Na Jioni. } (AL-FAT-H 9)

Na Akasema Tena: {Basi Wale Waliomuamini Yeye Na Kumuheshimu Na Kumsaidia Na Kuifuata Nuru Iliyoteremshwa Pamoja Naye (Quran) Hao Ndio Wenye Kufaulu} (Al Aaraf 157)

5-Kupenda Na Kuwatukuza Ahli Baiti Watu Wanyumba Yake Walio Silimu Na Wakafuata Njia Yake, Na Kufahamu Wasia Wa Mtume Wetu Muhamad (S.A.W) Amesema : &"Nawakumbusha Kwaajili Ya Allah Kwa Watu Wanyumbani Kwangu Na Wakumbusha Kwaajili Ya Allah Kwa Watu Wanyumbani Kwangu.&" (Imepokewa Na Muslim)

Na Watu Wanyumbani Kwa Mtume (S.A.W) Ni Wale Masharifu, Kama: Wakeze Mtume (S.A.W) Na Watoto Wake Na Jamaa Zake Wakaribu, Walio Haramishiwa Kuchukua Sadaka Haifai Kuwatweza Wala Kuwatukana Kama Vile Haifai Kudai Kuwa Hawafanyi Madhambi Wala Kuwaomba Kinyume Na Allah.

6-Kupenda Maswahaba Wake Walio Muamini Na Wakamsadikisha Bila Kuwataja Kwa Ubaya Kwani Allah Amewasifu Katika Kitabu Chake.

7-Haifai Kuwasema Maswahaba Wake Kwa Ubaya Wale Waliomsadikisha Na Kumuamini Nao Ni Aliowasifu Allah Katika Kitabu Chake Aliposema: {Muhamad Ni Mtume WA Mwenyezi Mungu Na Waliopamoja Naye Ni Wenye Nyoyo Thabiti Mbele Ya Makifiri Na Wenye Kuhurumina Wao Kwa Wao. Utawaona Wakiinama Kwa Kurukuu Na Kusujudu (Pamoja), Wakitafuta Fadhila Za Mwenyezi Mungu Na Radhi Zake Alama Zao Zi Katika Nyuso Zao Kwa Taathira, (Athari) Ya Kusujudu} (Al Fathu: 29)

Na Akasema Mtume(S.A.W) Kuwahusu: &" Msiwatukane Maswahaba Wangu, Msiwatukane Maswahaba Wangu, Naapa Na Yule Ambaye Nafsi Yangu Iko Mikononi Mwake Kama Mmoja Wenu Atatoa Mfano Wa Dhahabu Kiwango Cha Mlima Uhud Hawezi Kufika Kibaba Cha Thawabu Zao Wala Nusu Yake &" (Imepokewa Na Muslim)

Na Maswahaba Bora Zaidi Ni Makhalifa Wanne Walioongoka; Abubakar Na Umari Na Uthmani Na Alii (R.A) Amesema Allah Mtukufu: { Na Wale Waliotangulia Wakawa Wa Kwanza Katika(Uislamu)-Muhajirina Na Answari, Na Wale Waliowafuata Kwa Mwendo Mzuri – Mwenyezi Mungu Atawapa Radhi, Nao Wamridhie (Mwenyezi Mungu Kwa Hayo Mazuri Atakayowapa) Na Amewaandalia Mabustani Yapitayo Mito Mbele Yake, Wakakae Humo Milele. Huku Ndiko Kufuzu Kukubwa. } (At Tawba 100)

Wote Hawa Walifikisha Walioyapokea Kutoka Kwa Mtume (S.A.W) Mpaka Ikatufikia Nasi Elimu Ya Dini.



Tags: