MaaNa ya: {Na Mwenyezi Mungu aNa majiNa mazuri mazuri}

MaaNa ya: {Na Mwenyezi Mungu aNa majiNa mazuri mazuri}

MaaNa ya: {Na Mwenyezi Mungu aNa majiNa mazuri mazuri}

MajiNa ya Allah yote Ni majiNa mazuri, Na Allah ameyasifu katika quraNi kuWa yote Ni majiNa mazuri, akasema: {Na Mwenyezi Mungu aNa majiNa mazuri mazuri; muombeNi kWayo. Na WaacheNi Wale WaNaoharibu utakatifu WA majiNa yake. KaribuNi hivi WatalipWa Yale WaliyokuWa Wakiyatenda}. [Al aaraf: 180]

MajiNa haya hayakupata uzuri kWasababu ya kutamkWa, bali yamepata uzuri kWasababu yaNaonesha sifa zake zilizo kamilika, majiNa yake Allah yote Ni majiNa ya sifa nzuri ya shukraNi Na utukufu Na sifa, kWasababu hiyo ndio yakaWa mazuri, Na sifa zake zote Ni sifa za ukamilifu Na utukufu, Na vitendo vyake vyote Ni hikima tupu Na rehema Na maslahi ya uyu mWaNadamu Na uadilifu.

MiongoNi mWa vitu vya kuamiNi Ni kuamiNi majiNa yake Allah Mwenye nguvu Na utukufu, Na sifa zake Kama zilivyo katika quraNi Na suNa sahihi za Mtume (s.a.w) chiNi ya misingi miwili:

Qaida (msingi) WA kWanza: Kumthibitishia Allah kila kiNachostahiki Na utukufu Wake bila kupotosha Wala kuyafaNaNisha Na majiNa ya vitu vingine, bila kudadisi uhakika WA sifa zake zikoje, Kwa kulisadikisha neno lake Allah Mtukufu aliposema: {HakuNa chochote mfano Wake; Naye Ni Mwenye kusikia, Mwenye kuoNa} (Ash-shuura: 11)

Qaida (msingi) WA pili: Kufahamu maaNa ya sifa zake Na kuthibitisha sifa ambazo ziNaambataNa Na majiNa yake bila kujaribu kutaka kujua ziko vipi amesema Allah Mtukufu: {Mwenyezi Mungu aNajua yaliyo mbele Yao Na yaliyo nyuma Yao. Wala Wao haWawezi kumjua (Mungu) vilivyo} (Taha 110)

Amekwisha eleza Allah Mtukufu lengo la kujieleza Kwa Waja Wake, Kwa majiNa yake mazuri Na sifa zake za juu, lengo Wamuabudu yeye Kwa haya majiNa. Kama alivyo sema Allah Mtukufu: {“Sema;” muombeNi (mwenyezi mungu) Kwa jiNa la Allah au muombeNi Kwa jiNa la Rahman; Kwa jiNa lolote mNalomwita (katika haya itafaa); kWaNi aNa majiNa mazuri mazuri} (Al-israi: 110)

Amesema Allah Mtukufu: {Na mwenyezi mungu aNa majiNa mazuri mazuri; muombeNi kWayo. Na WaacheNi Wale WaNaoharibu utakatifu WA majiNa yake. KaribuNi hivi WatalipWa Yale WaliyokuWa Wakiyatenda}. (Al-a’araf:180)

MaaNa ya muombeNi:

Kuomba dua kupitia majiNa yake Allah mazuri, iNakusanya aiNa mbili za dua: dua kuomba haja, Kama kauli ya mja akisema:’ ewe Allah Nipe! ewe Mwingi Wa rehema Ni rehemu, ewe Mkarimu Ni kirimu, Na aiNa ya pili ya dua Ni kushukuru Na kumtukuza Na kumWabudu kama kumtukuza Allah kWa majiNa yake Na sifa zake bila kumuomba.Na kushukuru kuNakuWa kWa moyo au kWa ulimi, kumshukuru Allah MkubWa Alie juu Mwenye majiNa mazuri mazuri, Na sifa za juu.

Na maaNa ya WaacheNi Wale WaNaoharibu:

Kuaribu katika majiNa ya Allah Mwenye nguvu Na cheo: Ni kukataa Na kukanusha chochote kilichothibiti katika kitabu chake Allah Mtukufu, au kufaNaNisha majiNa yake Allah Na majiNa ya viumbe vyake, au kumuita Na kumsifu Kwa sifa Na majiNa yasiyo lingaNa Naye katika sifa Na majiNa ambayo hayaNa hoja katika maneno ya Allah Na suNa zake Mtume (s.a.w)



Tags: