Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.

Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.

Mwenyezi Mungu MkusudiWa

Hakika yeye Ni Mwenyezi Mungu MkusudiWa. {Sema: Yeye Mwenyezi Mungu Ni Wa pekee. Mwenyezi Mungu MkusudiWa. } (Al-ikhlas: 1-2)

“MkusudiWa” Aliye kamilika katika MajiNa Yake Na Sifa zake, haumtokei upungufu Wala kasoro.

“MkusudiWa” MkWasi (Tajiri) Aliyejitosheleza hahiitajii yeyote katika Waja Wake, Na Waja wote WaNamuhitajia yeye. {Naye ndiye aNaye lisha Wala halishwi} (Al-aNam: 14)

“MkusudiWa” Mola Mwenye kupanga vitu Na Mfalme Mwenye kuendesha mambo.

“MkusudiWa”…ANayekusudiWa Na viumbe Wake wote katika haja zao zote Na mambo Yao yakidharura, kWa ukamilifu Wake katika dhati yake Na majiNa yake Na sifa zake Na vitendo vyake.

“MkusudiWa” Nyoyo zimemuelekea yeye katika haja zao Naye akazipatia kila zilizo omba bila kuzinyima, Na zikamuomba katika haja zao akazifariji Na kuziondolea matatizo zao. Na kukubali maombi dua zao. Walimuomba Waliomkata akaWaunga, Na Walimuelekea wenye hofu akaWapa amaNi, Na Walimtaraji wenye kumpwekesha akaWafikisha, Walimuomba wenye matatizo akaWaondolea, Na WalishikamaNa Naye Waja Wake akaWainua daraja Allah Aliyetukuka.

Hakika yeye Ni Allah MkusudiWa…Tags: