Allah ni Mrithi

Allah ni Mrithi

Allah Ni Mrithi

Hakika yeye Ni Allah mrithi: {Na Sisi ndio tuNao huisha Na tuNao fisha. Na Sisi ndio Warithi.} (Al-hijri: 23)

“Mrithi” … Ambaye atarithi ardhi Na vilivyomo, hakutabaki yeyote ILA yeye Aliyetukuka,

“ Mrithi” … Atakaye baki baada ya Waja Wake; kWa ukamilifu Wa ufalme Wake, kWa ufalme Wake Watarudi Wafalme wote, aNahofisha mwenye kudhulumu Na kupita mipaka Na kufanya ujeuri kWamba marudio Ni kWake Allah kWasababu yeye Ni Mrithi baada ya kufa viumbe vyote.

“Mrithi”… ANaWahimiza Waja Wake kutoa katika njia zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, mali itaisha Na umri utakwenda, Na marejeo Ni kWake Allah Mrithi.

“Mrithi”… ANaWahadharisha Waja Wake Na kuacha kumshukuru, kWasababu asili ya neema Ni kWake Na marejeo yake Ni kWake pia.

“Mrithi” ANarithi ardhi Na vilivyomo, kWasababu kila mwenye kubakia baada ya kuondoka mwengine Ni mrithi. {Na Sisi ndio tumekuWa Warithi Wao} (Al-qasasi: 58)

Hakika yeye Ni Allah Mrithi…Tags: