Allwah Aliyetukuka

Allwah Aliyetukuka

AllWah Mtukufu mshindi

AllWah Aliyetukuka:

Allah Aliyetukuka... Mwenye Kuabudiwa Na Mwenye Kusifiwa …

Zinamsabihi Mbingu Na Vilivyomo Ndani Na Ardhi Na Vilivyomo …

Na Usiku Na Vilivyomo Na Mchana Na Vilivyomo Vyote Hivo Vinamsabihi Na Kumtakasa.

Anaye Mjuwa Allwah Zaidi Ndiye Anaye Muogopa Sana.

Amesema Allah: {Na Hakuna Chochote ILA Kinamsabihi (Mwenyezi Mungu) Kwa Sifa Zake Njema Lakini Nyinyi Hamfahamu Kusabihi Kwazo} (Al-Israi: 44)

&"Allwah’’ ... Jina Linye Kujulikana Sana Hushinda Yanayo Julikana Yote…Nyoyo Zinamjuwa Na Nafsi Zinamyenyekea.

&"Allwah’’ ... Anaabudiwa Na Nyoyo, Na Roho Zinatumai Kupata Msamaha Wake, Na Vilevile Viumbe Hupumbaa Kwa Kumtaja Yeye.

&"Allwah’’ ... Ameweka Kwenye Nyoyo Zawenye Kumuabudu Umbali Mbali Na Farakano Na Ufukara WA Kimaumbile Hazipati Tangamano Wala Kutosheka Illa Mja Anapo Mtegemea Mwenyeezzi Mungu Mtukufu.

&"Allwah’’ ... Ni Jina La Dhati La Yenye Kusifika Kwa Sifa Zote Njema.

Haja ya Waja Kwa AllWah mtukufu:

Kila Zawadi Isiokua Imani Chamalizika, Na Kila Tegemeo Na Msaada Usiokua Mwenyeezzi Mungu Unapomoka.

Mja Anahaja Ya Pakukimbilia Na Pakutegmea Penye Kumpa Amani Anapokereka Au Anapodhikika, Na Hayo Ndio Maumbile Yake, Kwa Hivyo Anahaja Na Mola Wake Katika Hali Zake Zote, Hali Yakuenda Mbio Kwa Ajili Yakutafuta Radhi Zake, Kwasababu Yeye Ni Mwenye Kukutana Naye..

Mja Anapomuhitajia Allwah Na Akatekeleza Yanayo Mpasa, Na Akayakinisha Yaliyoko Kwa Mwenyeezzi Mungu Na Kasubiri, Mwenyeezzi Mungu Humjalia Akawa Ni Katika Viongozi Wa Viumbe, Akawa Ni Imamu Mwenye Kufuwatwa: {Na Tukaweka Miongoni Mwao Maimamu Wenye Kuongoza Kwa Amri Yetu Waliposubiri Na Wakawa Na Yaqini Na Aya Zetu. } (As-Sjdah 24), Kwahiyo Allwah Amejalia Subira Na Yaqini Kuwa Ndizo Sababu Za Uongozi Katika Dini.

Na Viumbe Wametiwa Maumbile Kufungamana Na Mwenyeezzi Mungu (S.W) Na Vilevile Maumbile Ya Kumpenda Mwenye Kuwatendea Wema Na Mwenye Fadhla Juu Yao, Naye Ni Mwenyeezzi Mungu.

Utukufu WakumjuWa:

Ubora Wa Kujuwa Unetgemea Kijulikanacho,Wala Hakuna Kilicho Kitukufu Kuliko Mwenyeezzi Mungu(S.W)Na Kujuwa Sifa Zake Na Majina Yake Na Kinacho Pasishwa Na Hikma Yake Na Haki Yake Juu Ya Viumba Vyake(S.W), Ndipo Ikawa Kumpokesha Yeye Ni Kiiini Cha Dini, Na Ikawa Karibu Na Thuluthi Ya Quran Ni Maneno Wazi Kuhusu Kumpokesha Mwenyeezzi Mungu.

Na katika ukarimu Wa MwenyeEzzi Mungu Kwa mja Wake Ni kumsahilishia kumjuWa yeye.

Na kuNa Kwa kila kitu Alama yake :

Mwenyeezzi Mungu Ameweka Kwa Kila Kitu Alicho Kiumba Alama Yenye Kuonyesha Kuweko Kwake Na Umoja Wake Na Ukamilfu Wake Na Utukufu Wake Na Ukuu Wake (Sw), Kamwe Ameamrisha Tuziangalie Dalili Hizi Na Tuzifikirie, Na Akatujulisha Kwamba Hizo Ni Alama (Za Hayo) Kwa Wenye Bongo Na Akili Za Wanavioni Wajuzi Wenye Kufikiri..

Hebu Tuzunguke Kwenye Baadhi Ya Aya Za Quran Kwaharaka Haraka Kwa Wenye Akili Zenye Kuwapeleka Akili Zenye Kuwaita Kwenye Kumuamini Mwenyeezzi Mungu Mwenye Kukusudiwa Kwa Haja Zote, Amesema Mwenyeezzi Mungu Mtukufu: {Na Katika Ardhi Kuna Alama Zenye Kuwafaa Wenye Kuyaqinisha, Na Jee Hamujitizami Wenyewe?} (Ad-Dhaariyat 10-21)

Akasema Allah Mtukufu; {WA Ambie Tizameni Kuna Nini Mbinguni Na Ardhini} (Yunus 101)

Amesema Allwah Mtukufu { Hakika Mola Wenu Ni Allwah Alie Umba Mbingu Na Ardhi Kwa Siku Sita Kisha Akalingana Juu Ya Arshi, Ayapeleka Mambo, Hapatakuwa Na Muombezi Illa Baada Ya Idhni Yake Huyo Ndie Allwah Mola Wenu Muabuduni Hamuwaidhiki.Marejeo Yenu Nyote Ni Kwake, Hiyo Ni Ahadi Ya Mungu Ya Kweli Yeye Ndie Anaye Anza Kuumba Kisha Anakuregesha Tena Ili Awalipe Wale Walio Amini Na Wakafanya Mema Kwa Uwadilifu, Na Walio Kufuru Wana Vyakunywa Vya Maji Moto Mno Na Adhabu Ngumu Kwa Waliokua Wakiyatenda. Yeye Ndie Ambaye Alilijalia Jua Likawa Miangaza Na Mwezi Ukawa Nuru Na Akaukadiria Mashukio Ili Mupate Kujuwa Idadi Ya Miaka Na Hisabu Mwenyeezzi Mungu Hakuumba Hayo Illa Kwa Haki, Anazipambanua Dalili Kwa Wenye Kujuwa.Hakika Katika Kutafautiyana Usiku Na Mchana Na Kwenye Alivyo Viumba Mwenyeezzi Mungu Mbinguni Na Ardhini Kuna Alama Nyingi Kwa Watu Wenye Kumcha Mungu. } (Yunus 3-6)

Asema Allwah Mtukufu { Hakika Katika Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Na Kutafautiyana Usiku Na Mchana Kuna Alama Nyingi Kwa Wenye Akili, Wenye Kumtaja Mwenyeezzi Mungu Kwakusimama Na Kwakukaa Na Juu Za Mbavu Zao, Na Wafikiri Kuhusu Kuumbwa Mbingu Na Ardhi (Mpaka Wakasema)Ewe Mola Wetu Hukuyaumba Haya Kwa Batili Umetukuka Tuhifadhi Na Adhabu Ya Moto .} (Aal Imran 190-191)

Na Akasema Tena Allwah Mtukufu: {Na Katika Kuumbwa Kwenu Na Kwenye Hayawani Alio Waeneza Kuna Alama Kwa Wenye Yakini.} (JATHIYAH: 4)

Akasema Allwah Mtukufu; {Je! Hawatembei Katika Ardhi Wakawa Na Akili Zakufahamia Au Maskio Ya Kusikizia} (Al-Haj: 46)

Akasema Allwah Mtukufu; {Je! Hawakuangalia Mbingu Zilizo Juu Yao Tumezijengaje Na Tukazipampaje! Wala Hazina Nyufa! } (QAF: 6)

Akasema Allwah Mtukufu; {Kwa Hakika Kwenye Hayo Kuna Alama Kwa Wenye Akili} (Taha: 54)



Tags: