HAJA YA WAJA MAFUKARA KWA MOLA WAO MKWASI

HAJA YA WAJA MAFUKARA KWA MOLA WAO MKWASI

HAJA YA WAJA MAFUKARA KWA MOLA WAO MKWASI

Enyi Waja Wangu

Alisema Mtume (S.A.W) Kwenye Alilolipokea Kwa Mola (S.W) Kwamba Alisema: &"Enyi Waja Wangu Hakika Mimi Nilijiharamishia Dhulma Na Nikaharamisha Kati Yenu Basi Msidhulumiane. Enyi Waja Wangu Nyote Mmepotea Illa Niliemuongoza, Basi Niombeni Niwaongoze,, Enyi Waja Wangu Hakika Nyote Mna Njaa Ispokuwa Niliyemlisha Basi Niombeni Niwalishe, Enyi Waja Wangu Nyote Mko Uchi Isipokuwa Niliyemvisha Basi Niombeni Ni Wavishe, Enyi Waja Wangu Hakika Nyinyi Mnakosea Usiku Na Mchana Nami Na Samehe Madhambi Yote Basi Niombeni Niwasamehe, Enyi Waja Wangu Hamufikii Kunidhuru Mimi Wala Hamuwezi Kuninufaisha, Enyi Waja Lau Kama Wa Mwanzo Wenu Na Wamwisho Wenu, Na Mwanadamu Wenu, Na Jinni Wenu,Mungekuwa (Nyote) Kwenye Moyo Wa Mcha Mungu Mmoja Miongoni Yenu, Halingezidisha Hilo Kwenye Ufalme Wangu Chochote, Enye Waja Wangu Lau Kama Wa Mwanzo Wenu Na Wamwisho Wenu, Na Mwanadamu Wenu, Na Jinni Wenu,Mungekuwa (Nyote) Kwenye Moyo Wa Alie Muovu Mno Halingepunguza Hilo Kwenye Ufalma Wangu Chochote, Enye Waja Wangu Lau Kama Wa Mwanzo Wenu Na Wamwisho Wenu, Na Mwanadamu Wenu, Na Jinni Wenu Wangesimama Pamoja Wkaniomba Na Nikampa Kila Mmoja Alilo Liomba Halingepunguza Hilo Katika Nilivyo Navyo Illa Kama Inavopunguza Sindano Inapotiwa Baharini,Enye Waja Wangu Hizo Ni Amali Zenu Tu Nawadhibitia Kisha Niwalipe Zenyewe, Atakae Pata Kheri Namshukuru Mweneezzzi Mungum Na Mwenye Kupata Jengine Nasilaumu Kabisa Illa Mwenyewe .&" (Imepokewa Na Muslim)

Muhifadhi Allwah Naye Atakuhifadhi:

{Enyi Watu Hakika Nyinyi Ni Mafukara Kwa Allwah Na Allwah Ni Mkwasi Na Mwingi WA Shukran}(Fatri 15)

Imepokewa Kwa Abdillah Ibn Abas (R.A.A) Amesama Siku Moja Nilikuwa Nyuma Ya Mtume (S.A.W) , Akaniambia: &"Ewe Kijana Nakufundisha Maneno, Muhifadhi Allwah Atakuhifadhi, Muhifadhi Allwah Utampata Yuko Mbele Yako ,Ukiompa Muombe Allwah, Na Ukitaka Msaada Taka Kwa Allwah, Na Juwa Kwamba Watu (Umati) Lau Wangek’utaNa Ili Wakunufaishe Kwa Chochote Hawangekufaa Illa Kwa Kitu Alicho Kuandikia Mungu, Na Lau Kama Wangek’utaNa Kukudhuru Kwa Kitu Hawangekudhuru Illa Kwa Kitu Alicho Kuandikia, Kalamu Zishainuliwa Na Zakuandikwa Zimekauka.&" (Imepokewa Na Tirmiidh)Tags: